Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
RAIS Dkt. John Magufuli ametoa maagizo kwa Wakala wa Barabara ya Vijijini (TARURA)wilayani Kinondoni Dar es Salaam kujenga barabara inayounganisha Kinondoni Shamba na Biafra jijini.
Amesisitiza baada ya kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo Rais ametaka ipewe jina la Rashid Mashaushi ambaye ni mjumbe wa nyumba kumi wa CCM mtaa wa Kinondoni Shamba ambaye ndie aliyetoa ombi la ujenzi wa barabara hiyo kwa Rais.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam baada ya kutoka kukagua ujenzi wa Msikiti unaojengwa katika Makao Makuu ya Baraza la Waislam Tanzania(Bakwata) ambapo pia alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa Kinondoni.
Hivyo akiwa anazungumza na wananchi hao ndipo Mjumbe wa CCM mtaa wa Kinondoni Shamba aliejitambulisha kwa jina la Rashadi Mashaushi alipomuomba Rais kuangalia namna ya kuwasaidia ujenzi wa barabara hiyo.
Baada ya Rais Magufuli kumsikiliza Mashaushi alitoa maagizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuchukua namba ya mjumbe huyo ili aweze kuwasiliana naye na kumuonesha eneo ambalo atanataka litengenezwe.
Rais akatoa agizo hapo hapo kwa Mfuko wa Barabara Kinondoni kuhakikisha wanaanza ujenzi wa barabara hiyo na ikikamilika kwa heshima ya mjumbe huyo wa CCM ipewe jina la Rashidi.
Awali Rashid wakati anazungumza mbele ya Rais amemueleza wananchi wa Kinondoni Shamba wanasumbuliwa na mafuriko kutokana na kuziba kwa mifereji ndipo akiomba pia kujengwa kwa barabara hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akimsikiliza mjumbe wa Nyumba Kumi wa Konondoni Shamba Bw. Rashidi Mohamed Mashaushi anayeeelezea kuhusu changamoto ya barabara na mfereji wa maji eneo lao baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018.PICHA NA IKULU.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...