Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
Aliyekuwa Nahodha wa Azam FC, Himid Mao Mkami ameiaga rasmi timu hiyo, baada yakupata nafasi kwenda kucheza Soka la kulipwa nchini Misri kwenye Klabu ya Petrojet inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo inayofundishwa na Aliyekuwa Kocha wa timu ya taifa ya Misri, Hassan Shehata.
Himid maarufu kwa jina la Ninja aliyekuwa na Azam FC tangu mwaka 2009, katika ukurasa wake wa Instagram ametumia nafasi hiyo kuaga Benchi la Ufundi, Makocha, Viongozi na Wafanyakazi wote wa timu hiyo iliyomaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL).
‘Nashukuru kufanya kazi pamoja kila siku kwa ushirikiano na timu ya Azam katika kupanda na kushuka, huzuni na furaha na bado mlikua bega kwa bega na mimi miaka yote, ni huzuni kusema kwa heri lakini haikuwa na jinsi’, ameandika Himid Mao.
Himid amesema alifanya maamuzi kwa kushirikiana na uongozi wa timu hiyo na kumruhusu alipoomba ruhusa yakutafuta changamoto mpya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...