Na Habib Mchange
Wananchi watambue kuwa, Mfuko wa Kuendeleza Zao la Korosho “Cashewnut Industry Development Trust Fund (CIDTF)" ni chombo  binafsi  ambacho kilinzishwa mwezi  Juni, 2010 na kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Miunganisho ya Wadhamini, sura ya 318. 
Ni Mfuko wa Wakfu tu kama ulivyo mifuko mingi binafsi na sio chombo cha Umma au Serikali. Wadau wa Korosho wa wakati huo waliamua kuanzisha Mfuko huo ili kushirikiana kwa pamoja katika ugharimiaji wa maendeleo ya zao la korosho ikiwa ni pamoja na utafiti, elimu kwa mkulima huduma za ugani, masoko na kuhamasisha ubora wa korosho.  
Kabla ya kuanzishwa Mfuko huu, miaka ya 1990, kulikuwa na Mfuko kama huo ambao uliitwa “Cashewnuts Industry Development Trust Fund”. Mfuko huo nao haukuanzishwa na Serikali bali ulikubaliana na Serikali kupata fedha za ushuru wa Korosho zilizokuwa zikisafirishwa nje ya Nchi kiasi cha 2% ya bei ya FoB (thamani ya mzigo uliouzwa kabla ya kusafirishwa). 

Lakini kutokana ubadhirifu mkubwa wa fedha zilizoingizwa katika Mfuko huo kutoka Bodi ya Korosho Serikali ikasitisha kuupa fedha Mfuko huo na mwanzoni mwa miaka ya elfumbili, Mfuko huo ulikufa ukiwa umepoteza fedha nyingi za umma kutokana na ushuru wan korosho.
Serikali ilipozuia wakulima wasitozwe ushuru kuanzia mwaka 2005, Wakulima, Wabaunguaji, Bodi ya Korosho, Halmashauri za Wilaya na Wawakilishi wa Serikali Kuu walikutana mwezi Mei, 2010,  na Randama ya Maelewano ya kuanzisha Mfuko wa Korosho mpya ambao jukumu lake lilikuwa ni kushughulikia maendeleo ya korosho nchini. 

Wadau hao walikubaliana pia, kuiomba Serikali Kuu kuwa fedha ambazo zilikuwa zinakusanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2006 kwa lengo la kusaidia viwanda vya ubanguaji korosho, ziinghizwe kwenye Mfuko huo. 
Fedha hizo zilikuwa zinakusanywa kwa kwa kuzingatia  marekebisho ya Sheria ya Korosho ya mwaka 1984 ambayo iliweka kiasi cha 10% ya ushuru kwa korosho ghafi kwenda nje ya nchi.  TRA ilitakiwa itoe 6.5% kwenda Halmashauri za Wilaya zinazolima Korosho na 3.5% kwenda Mfuko Mkuu wa Hazina. Kusoma yote BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...