Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Selemani Jafo amezitaka Taasisi za serikali zinazo shughulika na masuala ya ujenzi kuwa kinara kwa ubora wa kazi zinazotekelezwa na taasisi hizo.

 Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa akikagua ujenzi wa jengo la halmashauri ya Makambako mkoani Njombe linalo jengwa na kampuni ya  MZINGA CORPORATION.

Katika ukaguzi huo, jafo ameagiza kazi hiyo ifanyike kwa ubora wa hali ya juu ili kuliwezesha jengo hilo kudumu kwa miaka mingi. 

Waziri Jafo kabla ya kukagua ujenzi huo amepata fursa ya kutembelea shule ya sekondari Makambako ambapo serikali imetoa sh.Million 150 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili. 

Akiwa katika shule hiyo, Waziri Jafo amefurahishwa na kazi iliyofanywa na halmashauri kupitia kamati ya ujenzi ya shule ambapo mabweni hayo mawili yamekamilika kwa kutumia "Force account'.

Aidha Waziri Jafo amempongeza Mbunge wa Makambako Deo Sanga kwa jitihada kubwa anayo ifanya kuwaletea maendeleo wananchi wake wa Makambako.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Jimbo la Makambako Deo Sanga pamoja na viongozi wengine wakiwa katika ukaguzi wa ofisi za halmashauri ya mji wa makambako.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo  akiwapongeza viongozi wa Mji wa Makambako kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa mabweni ya wasichana katika sekondari ya makambako.
 Majengo ya halmashauri ya mji wa makambako yanayo endelea kujengwa.
Mbunge wa Jimbo la Makambako Mhe. Deo Sanga pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Jombe.  Mhe. Lucy Msafiri wakifurahia jambo wakati wa Ziara ya waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo Jimboni humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...