Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Josephat Kandege amepongeza usimamizi mzuri uliofanyika katika ukarabati na ujenziwa vituo vya afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Jijini Arusha.

Ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye ziara hivi karibuni ya kukagua maendeleoya ujenzi wa vituo vya afya vya Nduruma kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Jijila Arusha na Kituo cha afya cha Usa River Kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya
Meru, Jijini Arusha.

Mhe. Kandege amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa vituo vya afya Jijini Arusha, na kuwapongeza kwa usimamizi mzuri wa majengo yaliyojengwa ambayo ni imara na yanaendana na dhamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.

“Miradi ya ujenzi wa vituo vya afya katika Jiji la Arusha ipo vizuri na kazi inayofanyika inaridhisha ukilinganishwa na fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya nchini.

Mhe. Kandege ametoa maelekezo kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati ili huduma za afya ziweze kutolewa kwa wananchi.Amezitaka Halmashauri kutengeneza mazingira mazuri ya vituo vya afya nchini ikiwa ni pamoja na kuweka uzio, kupanda miti hasa ya matunda ili kutengeneza mandhari inayovutia kwa wagonjwa pindi wanapohitaji kuaptiwa huduma ya afya.

Akiongelea kuhusu vyumba vya kujifungulia wanawake wajawazito Mhe Kandege ameelekeza chumba cha kujifungulia kitenganishwe kila kitanda ili kuwa na usiri wamama mjamzito anapojifungua.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Josephat Kandege akikagua jengo akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Jiji la Arusha .
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Josephat Kandege akitoa maelekezo kwa uongozi wa Wilaya wakati akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Jiji la Arusha
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Josephat Kandege akipatiwa maelezo wakati akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Jiji la Arusha
Moja ya jengo lililojengwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Jiji la Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...