Na Elisa Shunda 
VIONGOZI na Wanachama wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameungana kwa pamoja na Katibu Mkuu Mstaafu wa jumuiya hiyo Anayemaliza Muda wake,Seif Shaban Mohamed kumpokea Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya hiyo Erasto Sima katika hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya jumuiya hiyo zilizopo Kariakoo jijini Dar es Salaam Ijumaa. 
Akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi Katibu Erasto Sima alisema kuwa mojawapo ya vipaumbele vyake atakavyoenda kuvisimamia katika uongozi wake kwa nafasi hiyo ya utendaji wa jumuiya hiyo ya wazazi taifa atahakikisha anawakumbusha watendaji wenzake wa ngazi ya chini kufuatilia kwa makini ulipaji ada ya wanachama waliomo ndani ya muiya hiyo,pia ataendeleza kwa kufanya usimamizi wa kutosha katika uangalizi wa mali na miradi yote iliyopo ndani ya jumuiya hiyo. 
 "Tunao wanachama wengi katika jumuiya yetu hivyo nitalisimamia suala hili wanachama wetu walipe mapema ada zao siyo hadi kipindi cha uchaguzi ndo watu waje wawalipie ada kwa kweli hilo silipendi ukiwa wewe ni mwananchama wetu ni heri ujilipie ada mwenyewe lakini pia nitahakikisha nasimamia mali za chama na miradi yotde iliyopo katika jumuiya yetu iendelee zaidi ya hapa ilipo ili kukiongezea chama chetu kipato cha ndani" Alisema Katibu Sima. 
Akizungumza kuhusu utofauti wa nafasi aliyokuwepo awali na hivi sasa Katibu Mkuu huyo wa Jumuiya ya wazazi CCM Taifa,Erasto Sima alisema kuwa kwa sasa yeye ni mtendaji hivyo atamshughulikia ipasavyo mtu yoyote atakayetaka kukwamisha utendaji kazi wake na majukumu yake yasiende vizuri.

 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Aliyemaliza Muda Wake,Seif Shaban Mohamed (kulia) akimlaki Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya hiyo,Erasto Sima (kushoto) baada ya kuwasili katika katika ofisi za makao makuu ya jumuiya hiyo yaliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam leo,kwa ajili ya makabidhiano ya ofisi.


 Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa,Erasto Sima (kushoto) akisalimiana na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi CCM Mkoa wa Pwani, Dk.Zainab Gama.

Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa,Erasto Sima (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Kibaha Mjini, Edwini Shunda aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Pwani,Jackson Kituka (kulia) baada ya kuwasili ofisini hapo. Kulia kwake ni Katibu wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Pwani,Gama Juma Gama.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Aliyemaliza Muda Wake,Seif Shaban Mohamed (kulia) akimkaribisha ofisini na kumkabidhi vitendea kazi Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya hiyo,Erasto Sima (kushoto) katika hafla fupi ya makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya jumuiya hiyo yaliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Elisa Shunda.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...