*Aagiza Waziri wa Viwanda, RC na Menejimenti wakae na kumpa taarifa leo jioni
*Asema tofauti ya viwango vya mishahara inatisha, ataka orodha ya watumishi
*Awataka watumishi walioko kazini, likizo wawe wastahimilivu

SERIKALI imesema hairidhiki na ubia unaoendeshwa kwenye Kiwanda cha Nguo cha Urafiki. Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo jioni (Ijumaa, Juni mosi, 2018) wakati akizungumza na mamia ya wafanyakazi wa kiwanda hicho mara baada ya kukagua mitambo mbalimbali kwenye kiwanda hicho.
“Serikali haturidhiki na ubia huu, na huyu mbia aelewe kwamba Serikali haturidhishwi na ubia huu wala kinachoendelea hapa kiwandani,” amesema huku akishangiliwa kwa nguvu na wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage aongoze kikao baina ya wabia hao na menejimenti ya kiwanda na apewe taarifa hiyo leo saa 12 jioni baada ya kufuturu.

“Ubia wenu hauna tija. Kwa hiyo wewe Msajili wa Hazina na huyo mwekezaji, nikitoka hapa, mbaki mfanye kikao na mnipe majibu leo saa 12 jioni. Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Mkuu wa Mkoa muongoze mjadala huo na nikitoka kufuturu mniambie maazimio yenu, na kama haiwezekani, mvunje kabisa ubia huo ili tujue hatuna mbia tutafute mbia,” amesema.

Waziri Mkuu amesema wabia wakuu wa kiwanda hicho ni Msajili wa Hazina na kampuni ya Changzhou State owned Textile Assets Operations kutoka China na kwamba Serikali ilipoamua kukaribisha uwekezaji ilitarajia kupata mtaji, teknolojia na ajira za kutosha lakini hali ya sasa ni kinyume kabisa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki cha jijini Dar es salaam baada ya kukagua kiwanda hicho Juni 1, 2018. Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi, Evarest Ndikilo. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati  alipozungumza nao kiwandani hapo, Juni1, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mhandisi Mkuu wa kiwanda cha nguo cha Urafiki cha jijini Dar es salaam, Khamis Mazugo (kushoto)  kuhusu mitambo ya kiwanda hicho iliyokoma kufanya kazi wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 1, 2018. Kiwanda hicho kimesimamisha uzalishaji tangu Desemba mwaka jana.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipita katika eneo zilipong'olewa mashine za kiwanda cha nguo cha Urafiki cha jijini Dar es salaam wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 1, 2018. Kiwanda hicho kimesimamisha uzalishaji tangu Desemba mwaka jana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Naibu Meneja Mkuu wa kiwanda cha nguo cha Urafiki, Shadrack Nkelebe kuhusu mashine za kutengeneza  nyuzi za pamba wakati alipokitembelea kiwanda hicho, Juni 1, 2018. Kiwanda hicho kimesimamisha uzalishaji tangu Desemba mwaka jana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...