Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ongezeko la watu katika miji mikubwa kuna changia sana katika uharibifu wa mazingira na matumizi makubwa ya mkaa.Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa.
Makamu wa Rais amesema “Mkaa ni Ghali Tutumie Nishati Mbadala”, kwani kiwango cha miti inayokatwa kwa ajili ya kutengeneza mkaa ni kikubwa na kinatisha.
“ Dar es Salaam peke yake inakadiriwa kutumia kati ya magunia kati ya 200,000 mpaka 300,000 yenye uzito wa kilo 50 kila moja ya mkaa kwa mwezi na inategemewa itaongezeka zaidi kutokana na kasi ya ongezeko la watu hasa kwenye miji ” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amewata Watanzania, Makampuni pamoja na Taasisi mbalimbali kuungana na Serikali kubadilisha jamii yetu kuanza kutumia nishati ya majani kwa namna ya mkaa na kuni kama vyanzo mbadala vya nishati endelevu.
Makamu wa Rais amesema kuwa kilele cha Siku ya Mazingira ni tarehe 5 Juni, 2018 ambapo dhima ya Kimataifa ni Kupiga Uchafuzi wa Mazingira unaotokana na Plastiki (Beat Plastic Pollution) lakini Tanzania imelekeza nguvu zake katika kuadhimisha siku hiyo kwa kuwataka Wananchi wake wabadilike badala ya kutumia mkaa ambao unasababisha ukataji mkubwa wa miti ni vyema kuanza kutumia nishati mbadala.
Mapema; Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba alisema kutokana na uhitaji na umuhimu wa kutunza mazingira Serikali, Wadau wa Maendeleo, Taasisi mbali mbali, Sekta Binafsi na Watungaji wa Sera kutafakari kwa pamoja na kuja na majawabu yatakayosaidia katika utunzaji wa mazingira na kuilinda miti.
Wakati huo huo;  Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Katarina Rangnitt amesema tangu mwaka 1972 changamoto za uharibifu wa mazingira hazikuwa za Kikanda tu bali ni kwa dunia nzima hivyo hili jambo linahitaji ushiriki wa Dunia nzima katika kupambana na uharibifu wa mazingira.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa  Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa  lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na kufanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimshukuru Profesa Mark Mwandosya kwa zawadi ya kitabu mara baada ya ufunguzi wa  Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa  lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na kufanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. 
 Balozi wa Sweden nchini Mhe. Katarina Rangnitt akihutubia wakati wa ufunguzi wa  Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa  lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na kufanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba  akihutubia wakati wa ufunguzi wa  Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa  lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na kufanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...