Na Heri Shaaban
MANISPAA ya Ilala wameibuka mabingwa wa jumla katika michezo yote ya mashindano ya umoja wa Shule za Msingi Umitashumta Mkoa wa Dar es Salaam na nafasi ya pili Wilaya ya Kinondoni na nafasi ya tatu Temeke.
Akizungumza Dar es salaam jana, Ofisa Michezo mkoa wa Dar es Salaam Hadoph Ally amesema wameunda kikosi cha mkoa chenye wachezaji 120 ambao watakwenda Mwanza kushiriki ngazi ya Taifa.
"Mashindano ya umitashumta ngazi ya mkoa yalishirikisha timu za wilaya tano Ilala, Temeke, Ubungo, Kinondoni na Kigamboni ambapo bingwa amepatikana katika mashindano hayo na tumeunda wachezaji 120 ambao wanasafiri kwenda kushiriki ngazi ya Taifa wakiambatana na viongozi wao 20 jumla 140,"amesema.
Kwa upande wake Ofisa Elimu Ilala Elizabeth Thomas amepongeza ushindi wa jumla katika wilaya yake.Amesema Ilala ni mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo imekuwa ikifanya vizuri Mashindano hayo na mwaka huu timu kutoka kutoka Dar es Salaam itarejea na vikombe vyote ngazi ya Taifa.
Amesema kamati ya Ilala iliwaanda vizuri wachezaji wao ndio siri ya mafanikio ya ushindi mnono .Amesema mazingira ya timu ya Ilala yalikuwa mazuri ndio yamewafanya Kufanya washinde.

OFISA ELIMU MSINGI MANISPAA ya ILALA Elizabeth Thomas (kushoto) akikabidhiwa kombe LA ushindi wa jumla mkoa Dar es Salaam ambapo ILALA wameibuka mabingwa na OFISA ELIMU Taaluma mkoa wa Dar es Salaam Janeth Nsunza Jana, katika ufungaji WA mashindano ya Umoja wa Shule za Msingi(UMITASHUMTA)wengine Mratibu wa Umitashumta ILALA Hamis Ngoda (PICHA NA HERI SHAABAN)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...