Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza, amewataka makandarasi wanawake
wote nchini kufanya kazi kwa kujiamini na kutooneana wivu katika maeneo
yao ya kazi.
Amesema kuwa lengo la Serikali ni kuwawezesha makandarasi wanawake kufikia madaraja ya juu ya ukandarasi ili kuwawezesha kuchukua kandarasi kubwa, na hivyo kuinua kipato chao kitakachopelekea kuondokana na umaskini katika familia na jamii zinazowazunguka.
Ametoa wito huo mkoani Iringa, wakati akifungua mafunzo elekezi kwa makandarasi wanawake wa mikoa ya nyanda za juu kusini katika ushiriki wa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara hapa nchini na kusema kuwa mashindano yao yawe ni ya kutimiza wajibu na siyo kushindana katika kuvaa wala kusuka.
"Nataka mwanamke wa kitanzania ujiamini na kusimama vyema na kusonga mbele kwani sifa yetu kubwa ni kuhakikisha tunatunza familia kwa hali yoyote, wajibikeni ipasavyo katika kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara bila woga wowote", amesema Mhe. Masanze.
Aidha Mhe. Masenza, amesisitiza umuhimu wa makandarasi hao kujaza nyaraka za zabuni na mikataba wenyewe ili kuepukana na utapeli na baadhi ya watu wanaojidai wanawasaidia shughuli hizo. Amewataka makandarasi wanawake hao kufanya kazi kwa ushirika na sio mmoja mmoja ili kuweza kumiliki kampuni au vikundi vya ujenzi ambavyo vitawasaidia kupata zabuni za miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa hapa nchini.

wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza, akihutubia makandarasi wanawake
kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini (hawapo pichani), wakati wa
ufunguzi wa mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo katika ushiriki wa kazi
za ujenzi na matengenezo ya barabara, yaliyofanyika mkoani humo.
Mratibu
wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wanawake kutoka Sekta ya Ujenzi,
Mhandisi Rehema Myeya, akizungumza wakati akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa
Iringa, Mhe. Amina Masenza (kulia), kufungua mafunzo elekezi ya
kuwajengea uwezo makandarasi wanawake katika ushiriki wa kazi za ujenzi
na matengenezo ya barabara, yaliyofanyika mkoani humo.
Baadhi
ya makandarasi wanawake kutoka mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma,
Rukwa na Katavi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza
(hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi ya kuwajengea
uwezo katika ushiriki wa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara,
yaliyofanyika mkoani Iringa.
Meneja
wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Iringa Mhandisi Daniel
Kindole, akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza, mara
baada ya kufungua rasmi mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo kwa
makandarasi wanawake katika ushiriki wa kazi za ujenzi na matengenezo ya
barabara, yaliyofanyika mkoani Iringa.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza akiwa katika picha ya pamoja na
makandarasi wanawake kutoka mkoa wa Iringa baada ya kufungua mafunzo
elekezi ya kuwajengea uwezo katika ushiriki wa kazi za ujenzi na
matengenezo ya barabara, yaliyofanyika mkoani humo.Imetolewa na Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...