Na Mwandishi wetu
Mchezaji wa mpira meza wa Tanzania, Sara Alidina ameingia hatua ya mashindano ya mikoa ya Kenya iliyopangwa kuanza wiki ijayo baada ya kushinda medali ya fedha katika hatua ya awali.
Sara aambaye anasoma katika shule ya Aga Khan Academy Mombasa, amejumuishwa katika timu ya Mvita ambayo pia inaundwa na wachezaji wawili kwa ajili ya mashindano mkoa.
Sara alianza michuano hiyo kwa vishindo baada ya kumchapa Rachel Thomas kwa seti 2-0 (11-4, 11-6) na baadaye kupata ushindani mgumu kutoka kwa Elizabeth Ochieng ambaye alianza kwa kushinda kwa 15-14 kabla ya kumbadilishia kibao na kuibuka na ushindi kwa seti mbili zilizobaki kwa 11-5 na 11-4).
Sara aliendelea kutamba katika mashindano kwa kumchapa Christine Augustine kwa 2-0 (11-4, 11-6) na baadaye kushinda dhidi ya Maliha Haji kwa 2-0 (11-4, 11-5) na kupoteza kwa 2-0 dhidi ya Rachel Simon kwa 8-11 na 9-11.
Pamoja na kushindwa dhidi ya Rechal, Sara alifuzu hatua ya robo fainali na kushinda mechi dhidi ya Eliza Wanjiru kwa 2-0 (11-4, 11-4) na kushinda tena kwa 2-0 katika hatua ya nusu fainali dhidi ya Catherine Okoth kwa 11-4 na 11-6. Hata hivyo alikumbana na kigindi katika fainali kwa kufungwa 2-1 dhidi ya Krupa Vyas kwa 11-8, 9-11 na 11-7.
Akizungumza kwa njia ya simu, Sara alisema kuwa mashindano hayo yalikuwa magumu sana na kushukuru Mungu kwa kufuzu hatua ya mashindano ya mikoa.
“Lengo ni kutwaa ubingwa pamoja na kupata ushindani mkubwa, mechi nyingi zilikuwa ngumu na hasa ukingatia kuwa nacheza na wachezaji wakubwa zaidi yangu. Hii imesababisha kuchoka na kufungwa katika hatua ya fainali,” alisema Sara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...