Na Frankius Cleophace Tarime

MWENYEKITI wa Mtaa wa Mtaa wa Bugosi Kata ya Nyamisangura Mjini Tarime mkoani Mara Zacharia Ghati amevamiwa akiwa njiani na watu wanaodhaniwa kuwa vibaka na kumshambulia kwa kutumia vitu vyenye ncha kali.

Pia vibaka hao walikuwa na nondo na marungu ambayo waliyatumia kumshambulia nayo,hivyo kumsababishia maumivu makali na kisha wakampora fedha Sh.320,000.

Akizungumza na Michuzi Blog akiwa amelazwa katika Hospitlai ya Mji wa Tarime Mwenyekiti huyo amedai tukio hilo limetokea Saa Nne ambapo ameporwa pia kitamburisho chake cha kazi na cha mpiga kura pamoja na kumsababisha maumivu.“Nilikuwa nimesindikiza mmoja wa wananchi wangu alienda kwenye harusi kwa ajili ya kuchinjia mama mkwe sasa kipindi tunarudi nilipofika mtaani kwangu nilipigiwa simu na mwenyekiti wa Mtaa.

"Hivyo wananchi tukaachana na kipindi naenda nilikutana na watu wawili wakanisimamisha wakaanza kunishambulia na panga na kisha wengine kama wanne wakaongezeka ndio wakaanza kunishambulia kwa virungu na nondo,” amesema . Mmoja wa wananchi Chacha Masero aliyekuwa ameambatana na Mwenyekiti huyo kabla ya kutokea kwa tukio hilo amesema saa tatu wakiwa nyumbani baada ya kutoka kwenye harusi Mwenyekiti huyo alipigiwa Simu na Mjumbe wa Mtaa.

Ameongeza hivyo alimua kuondoka peke yake na baada ya muda alipokea taarifa za Mwenyekiti huyo kuvamiwa na vibaka. “Mie nilipopata taarifa hizo nilikwenda Polisi na kisha tukafanya utaratibu wa kumleta hospitali mpaka sasa anaendelea na matibabu japo ameumizwa sana Mwenyekiti wetu,” amesema Chacha.

Nao wananchi wa Mtaa wa Bugosi Kata ya Nyamisangura wameiomba Serikali likiwemo Jeshi la Polisi kuendelea kusimamia ulinzi huku wakichukuliwa hatua kali vibaka wanakamatwa na kufaamika katika mitaa huska.“Kuna vibaka wanafaamika kabisa lakini wanalindwa na baadhi ya viongozi kwa sababu ya undugu, tunaomba washughulikiwe,” amesema mmoja wa Wananchi.

Aidha Diwani wa kata ya Nyamisangura Bashir Abdallah amethibitisha kushambuliwa kwa mwenyekiti huyo. Hivyo ameliomba Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi maeoneo yote na kuwahi kwa wakati pindi tukio linapotokea popote. Abdallah amesema kuwa Polisi wamekuwa wakichelewa katika eneo la tukio pale wanapopigiwa simu za haraka hivyo kuna haja kubwa ya jeshi hilo kulifanyia kazi suala hilo.

“Ndo Maana kukaundwa kanada Maalumu Tarime Rorya siyo kwa sababu ya vita vya koo ni pamoja na kulinda wananchi na mali zao ili wananchi wasiishi kwa hofu,” amesema Diwani.

Diwani wa kata ya Nyamisangura Bashir Abdallah akiwa katika Hospitali ya Mji wa Tarime akijulia hali ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugosi Zacharia Chacha Ghati aliyevamiwa na Vibaka na kushambuliwa na Vitu Vyenye Ncha kali zikiwemo Nondo na Vilungu na kumsababishia Maumivu Makali.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugosi kata ya Nyamisangura Zacharia Chacha Ghati akiwa amelazwa katiko Hospitali ya Mji wa Tarime Mkoani Mara kwa ajili ya Matibabu.
Chacha Masero Mkazi wa Bugosi akisimulia juu ya tukio hilo kwani alikuwa na Mwenyekiti kabla ya kutokea kwa tukio hilo.
Diwani wa kata ya Nyamisangura Bashiri Abdallah akidhibitisha uwepo wa Tukio hilo katika kaya yake huku akiomba jeshi la Polisi kujimalisha ulinzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...