Na Mwandishi wetu,
WATAFITI waliokuwa wakifanyia utafiti mada kuhusu ukuaji bora wa miji nchini Tanzania, wamekamilisha kazi hiyo na kuwasilisha katika mkutano mkubwa wa wadau chini ya mwavuli wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) siku ya Ijumaa tarehe 8 Juni 2018.
Katika mkutano huo ambao ulifunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dkt. Tausi Kida, ilielezwa kuwa Tanzania Urbanisation Laboratory (TULab) ilikuwa na mafanikio makubwa kutokana na kuonesha njia bora ya ukuaji wa miji nchini Tanzania kwa kuzingatia uchumi wa viwanda katika tafiti zake tatu.
TULab ilibuniwa mwaka jana kufuatia uchambuzi wa hoja ya Better Urban Growth in Tanzania ambayo ilijengwa katika kuhakikisha kunakuwepo na uelewa na kuuchochea mazungumzo ya kisera juu ya mabadiliko muhimu yanayotarajiwa katika kuelekea nchi yenye majiji makubwa yanayoshindana.
Mkutano wa mwishoni wa wiki uliitishwa kwa ajili ya kuona kilichojiri katika tafiti tatu kabla ya utafiti mwingine wa nne kufanyika, baadae mwaka huu.
Utafiti huo umelenga kutoa majibu kwa maswali yanayohusu maendeleo ya miji nchini Tanzania ambapo wadau wanatakiwa kuona.
Dkt. Kida alishukuru Wizara ya Fedha na Mipango kwa kukubali kuwa mwenyekiti wa jukwaa hilo lenye umuhimu kwa maendeleo ya taifa.
Septemba mwaka jana kulianzishwa tafiti tatu ambazo zilichangiwa vyema na wajumbe na sasa mkutano huo ulikuwa unatoa taarifa za mwisho kuhusu nini wamekibaini katika tafiti hizo tatu.
Utafiti wa kwanza ulilenga kuelewa ugharimiaji wa miundombinu na huduma katika majiji makubwa 6 nchini Tanzania. Utafiti wa pili ulichunguza uhusiano kati ya serikali kuu na serikali za mitaa na namna uhusiano huo unavyo athiri ugharamiaji wa miundombinu na utoaji wa huduma katika miji, na utafiti wa tatu ulilenga kuibua taarifa na takwimu ambazo zilikuwa hazijabainika hasa katika masuala ya maji.
pekee au watu binafsi pekee bali zinatakiwa kufanywa kwa ushirikiano.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi
Kida akitoa neno la ukaribisho wakati wa mkutano wa mabaara kuhusu
mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji yaliyopangwa uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa mkutano huo, Dkt. Lorah Madete akitoa neno la ufunguzi wakati wa
mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Dr. Idda Swai akiwsailisha utafiti juu ya
uhusiano kati ya Serikali kuu na serikali za mitaa na athari zake katika
kutoa huduma kwa wananchi wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya
Tanzania kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mratibu
wa Maabara inayoshughulikia mabadiliko kuelekea miji Tanzania (TULab)
kutoka ESRF, Mussa Martine akiwasilisha mada kuhusu huduma za tafiti za
kifedha kwenye miji wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania
kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano
wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mtafiti
Mshiriki kutoka Taasisi inayoshughulikia makazi ya watu katika Chuo
Kikuu cha Ardhi, Dr Nathalie Jean-Baptiste akiwasilisha mada kuhusu
utafiti uliofanywa wa maisha ya kila siku ya wananchi kwenye miji ya
Tanzania wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania kuelekea kwenye
miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini
Dar es Salaam.
Bw.
Anton Cartwright kutoka Taasisi ya Miji ya Afrika iliyopo Afrika
Kusini, akielezea mipangilio ya programu hiyo kuelekea mabadiliko ya
miji iliyopangwa wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania
kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano
wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi
Kida (kushoto) na Mwenyekiti wa mkutano huo, Dkt. Lorah Madete
wakijadiliana jambo wakati wa mkutano kuhusu mabadiliko ya Tanzania
kuelekea kwenye miji iliyopangwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano
wa ESRF jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...