Inaweza kukuwia vigumu kuamini, lakini ndiyo hivyo tena, akiwa anatimiza umri wa miaka 68, miaka 39 ya kuwepo kwenye fani za michezo na burudani, Mzee Juma Mbizo ameamua kuingia studio kwa mara kwanza na kufanya ‘kolabo’ na mwanae H-Mbizo.
Naam Mzee Mbizo amejitosa katika studio za Fire Music chini ya producer More Fire na kurekodi wimbo wa pamoja na H-Mbizo aliyepata kutamba na wimbo wa “Mchumba”.
H-Mbizo ambaye pia ni mwandishi mzuri wa nyimbo akiwa amewaandikia wasanii wengi akiwemo Snura kupitia wimbo “Majanga”, ameuambia mtandao huu kuwa kibao hicho alichoimba na baba yake kitaachiwa hewani mwezi huu.
Licha ya ukongwe wake kwenye game na utalaam wa kuandaa matamasha makubwa ya burudani, lakini Mzee Mbizo hakuwahi kuingia studio na kurekodi wimbo wowote ule na hii ndio hali itayofanya kazi hii alishoshirikishwa na mwanae iteke masikio ya mashabiki wengi wa muziki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...