Baada ya kuwadatisha washabiki katika maonyesho mawili makubwa kule Regensburg Festival na Birkenreid festival Ujerumani sasa kamanda Ras Makunja anakipeleka kikosi kazi cha Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni katika onyesho kubwa la Mamling Festival nchini Austria ,onyesho hilo litafanyika siku ya jumapili Julai 8, 2018.
Akiongea na vyombo vya habari kiongozi wa bendi hiyo Ebrahim Makunja aka Kamanda wa FFU Ughaibuni Ras Makunja alisema Ngoma Africa band ni mali ya washabiki na ina kazi moja tu nayo kudatisha washabiki katika kila onyesho bila kuremba remba.
Bendi hiyo iliyojizolea umaarufu na maelfu ya washabiki kila kona duniani imejiwekea rekodi ya aina yake kuwa ni bendi ya mwanzo ya kiafrika kuimiri vishindo,na kudumu kwa miaka 24 ughaibuni na kufanikiwa kuwanasa washabiki wa kimataifa.
ungana nao at www.ngoma-africa.com
wape hi at www.facebook.com/ngomaafricaba nd
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...