Katibu wa Rais Ngusa Samike akimkabidhi Rehema Kadogosa ambaye ni Mama wa Mtoto Latifa Kadogosa (13) aliyelala kitandani kiasi cha Shilingi milioni tano (5,000,000/-) fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kumsaidia mtoto huyo ambaye ana matatizo ya kiafya jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Rais Ngusa Samike akimuangalia mtoto huyo Latifa Kadogosa(13) ambaye amepakatwa na Mama yake Rehema Kadogosa Mwenge jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Tawi la Benki ya CRDB Mikocheni Rehema Moyo akimkabidhi Kadi ya Benki Rehema Kadogosa mama mzazi wa Latifa Kadogosa mara baada ya kufungua Akaunti katika tawi hilo kwa ajili ya kutunza fedha hizo alizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na fedha nyingine atakazosaidiwa na wadau wengine. PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mie binafsi napenda sana juhudi za Rais wangu Dr magufuli anazozichukua kwa kujenga nchi yetu mie niko pamoja na ww na watanzania wote wako pamoja na wewe.
    Na pia tunakujali sana Rais wetu kwa kuwa na huruma na ww ndo kiongozi bora wa uigwa .Tuko pamoja mheshimiwa Rais wetu .
    Waheed sanya kutoka Zanzibar

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...