VETERANI wa timu ya soka ya Uingereza ya Liverpool, Sami Hyypia amewataka vijana Watanzania kuongeza bidii katika kuhakikisha kwamba wanafikia hatua za juu za uchezaji soka hivyo kupata nafasi ya kucheza Ulaya.

Pia amesema ni matumaini yake kuwa mamlaka za utoaji leseni hazitawazuia vijana kwenda Ulaya kujaribu bahati zao.Alisema hayo wakati wa kiliniki ya soka aliyoifanya kwa vijana wa Serengeti boys jana alipokuwa akishiriki nao katika mafunzo na mazoezi.

Alisema kwamba yeye hakuwa na kipaji kikubwa kuliko alivyoviona kwa vijana hao lakini ameweza kufikia hatua za juu kabisa za uchezaji wa soka kutokana na kujituma kwake.Alisema amewaambia vijana kuangalia zaidi juhudi kwani kipaji pekee hakitoshi kumfanya mtu kuwa gwiji katika soko.Alisema pamoja na mafundisho ya walimu ni kazi ya mchezaji mwenyewe kuona udhaifu wake uliopo na kuufanyia kazi ili aweze kuwa mwanasoka bora wa kutegemewa.

Akihojiwa mwanasoka huyo ambaye aliwika sana katika enzi zake alisema kwamba amefurahishwa na uchezaji wa timu hiyo hasa kwa pasi ndefu na kusema kwamba vijana wote wameonesha kuwa na vipaji vikubwa.Alisema hata hivyo kwamba amewaambia wachezaji awali kuwa na kipaji pekee hakutoshi lakini ni lazima mtu binafsi kufanyakazi ya ziada kuondoa udhaifu wake ambao binadamu wengi wanakuwa nao ili kuwa mahiri katika uchezaji.

Sami ambaye yupo nchini kuangalia michuano ya kombe la benki ya Standard Charted  inayofanyika leo na kushirikisha timu 32 zinazowania kwenda Anfield kuona mechi za msimu mpya timu ya Liverpool  ndani ya EPL na kuzungumza na magwiji na kupata nafasi ya kunolewa, amesema siri kubwa ya mafanikio ni kujituma kwa mchezaji pamoja na kwamba anakipaji na walimu wazuri.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba akimtambulisha Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kushoto) kwa timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakati wa kliniki ya soka iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akizungumza na kikosi cha timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakati wa kliniki ya soka iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba (kulia) pamoja na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakimsikiliza Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (hayupo pichani) wakati akiendesha kliniki ya soka kwa vijana wa Serengeti Boys iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...