Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii
Taasisi ya Uhasibu  Nchini (TIA) kimesema kuwa waombaji wa kozi mbalimbali katika chuo hicho wanaomba moja kwa moja kwa njia ya mtandao ikiwa ni kuwaondolea usumbufu kwenda vyuoni kwa kwa ajili ya udahili.

Akizungumza katika banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika moenesho ya 42 ya biashara ya  kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Mhadhiri wa Taasisi hiyo  Alex Marwa amesema kuwa  watakaotembelea maonesho ya sabasaba watasaidiwa  kufanya maombi  ya kujiunga  na chuo kwa njia ya Mtandao.

Amesema kuwa kwa waombaji wanaweza kuomba katika tovuti ya www.tia.ac.tz ambapo baada ya kuomba hapo atapata maelezo yote na kuunganishwa huduma nyingine za mahitaji ya chuo .

Amesema kuwa Chuo cha Uhasibu  kinaendelea kutoa elimu bora kwa ajili ya maendeleo ya taifa kutokana na kozi zilizopo katika kila mwaka wa masomo .

Marwa amesema kuwa hakuna usumbufu wowote utaokaojitokeza katika maombi katika njia ya mtandao.
 Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charle’s Kichere akitoa maelezo katika banda banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika moenesho ya 42 ya biashara ya  kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
 Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere akisaini kitabu cha wagene alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Taasisi ya Uhasibu katika moenesho ya 42 ya biashara ya  kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
 Ofisa wa Idara ya Bajeti ya Serikali wa Wizara ya Fedha na Mipango, Boniface Kilindimo akitoa maelezo ya bajeti kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya  Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere  akipata maelezo kuhusu Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi  na Ugavi (PSPTB) kutoka  kwa Ofisa Mwandamizi wa Masoko na Mahusiano ya Umma wa Bodi  hiyo Wataalamu wa Ununuzi  na Ugavi (PSPTB), Shamim Mdee alipotembelea  Banda la Wizara ya Fedha na Mipango  katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya  Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...