Meneja Uzalishaji wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Mhandisi Ben Lema (wa pili kulia), wakipeana mikono na Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni,Upendo Magashi katika hafla ambayo kampuni hiyo ilikabidhi jengo la wodi ya wazazi la hospitali ya wilaya hiyo pamoja na samani zake lililojengwa msaada kwa gharama ya shs milioni 87. Wengine ni baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo. Hafla ya makabdhiano ilifanyika Handeni, Tanga.
Meneja Uzalishaji wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Mhandisi Ben Lema na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Mgaya Twaha (kulia) wakikata utepe kuashiria uzinduzi na makabidhiano rasmi ya  jengo la wodi ya wazazi la hospitali ya Wilaya ya Handeni lililojengwa msaada kwa gharama ya shs milioni 87 na Tanga Cement. Anayeshuhudia ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Upendo Magashi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Mgaya Twaha akizungumza katika hafla ambayo Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC) ilikabidhi jengo la wodi ya wazazi pamoja samani zake la hospitali ya wilaya hiyo lililojengwa msaada kwa gharama ya shs milioni 87. Hafla ya makabidhiano ilifanyika, Handeni mkoani Tanga. Kushoto ni Meneja Kiwanda wa Tanga Cement, Mhandisi Ben Leman na kulia ni Katibu Tawala wa Handeni, Upendo Magashi.
Ofisa Mawasiliano wa  Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Helen Maleko (kulia) akizungumza katika hafla ambayo kampuni hiyo ilikabidhi jengo la wodi ya wazazi pamoja samani zake la hospitali ya wilaya hiyo lililojengwa msaada kwa gharama ya shs milioni 87. Hafla ya makabidhiano ilifanyika, Handeni, Tanga mwishoni mwa wiki. Wengine ni viongozi wa wilaya na kutoka TCPLC.   
Baadhi ya wananchi  na wafahanyakazi wa Hospitali ya Wilaya ya Handeni waliohudhuria hafla hiyo.
Viongozi wa kiserikali na kisiasa pamoja na maofisa wa Tanga Cement wakipiga picha ya kumbukumbu mbele ya jengo la wodi ya wazazi ya Hospitali ya Wilaya ya Handeni lililojengwa na kampuni hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...