Na Rhoda Ezekiel Kigoma

IMEELEZWA zaidi ya tani 160 za matumizi ya nishati ya  kuni na mkaa  hutumika katika  kambi za wakimbizi mkoani Kigoma kwa siku moja, kwa  matumizi ya kupikia.

Hivyo hali ina sababisha uharibifu wa mazingira katika maeneo yaliyokaribu na kambi hizo.Hayo yalibainika jana wakati wa  kilele cha Maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani ,  yaliyofanyika kimkoa katika Kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani humo.

Akizungumza  Mratibu wa mradi wa utunzaji wa mazingira  kambini CEMDO Tanzania Frank Kayegameni akitoa taarifa ya mradi huo amesema kutokana na  idadi kubwa ya wakimbizi  kambi ya Nyarugusu ambayo imesababisha uhitaji mkubwa wa matumizi ya mazao ya misitu.Amefafanuana  wakimbizi huenda kutafuta kuni nje ya kambi kwa kukata miti ambapo kwa siku inakadiriwa mtu mmoja anatumia kiasi cha kuni kilo moja na kambi inakadiriwa kuwa na wakimbizi 152,309 hivyo kusababisha  uharibifu mkubwa.

Amesema katika kupambana na hali hiyo Shirika la uhifadhi wa mazingira  na utunzaji wa mazingira kambini ( CEMDO) Tanzania,  kwa kushirikiana na Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR wameandaa utaratibu wa upandaji wa miti 1,425,223  katika Vijiji 13 vinavyozunguka Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kwa mwaka 2017/2018 , kugawa majiko banifu kwa kaya 9600 za wakimbizi.

Pamoja na majaribio ya ugawaji wa gesi  kwa kaya 3180 lengo likiwa ni kupunguza matumizi ya nishati ya mkaa na kuni  yanayosababisha uharibifu mkubwa wa mazingira pamoja na  kuboresha mazingira kutokana na uharibifu mkubwa wa uoto wa asili  unaotokana na ukataji miti ovyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea  Ndagala akipokea Maelezo ya Mazao ya mboga mboga yanayo limwa na wakimbizi Kambi ya Nyarugusu katika mradi wa utunzaji wa Mazingira
 Mmoja wa Wakimbizi akimuelezea Mkuu wa Wilaya namna wanavyo yatumia Majiko banifu kuhakikisha hawaharibu mazingira
 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko kanali Ndagala  akioneshwa na Afisa wa Shirika la CEMDO majiko banifu yanayotumia kuni chache kwa lengo la kutokomeza uharibifu wa mazingira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...