WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema taarifa ya Kongamano la Uchumi la Dunia la mwaka 2018 inaonesha kuwa Tanzania inaongoza kwa kuwa na uchumi jumuishi miongoni mwa nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Amesema hali hiyo, imetokana na Tanzania kufungua fursa za ujasiriamali ambapo kuna zaidi ya biashara milioni tatu zinazokuwepo kila mwaka, lengo la nchi ni kuhakikisha kuwa uchumi unakua na unamgusa kila Mtanzania hususan mwananchi wa kawaida.
Waziri Mkuu ameyasena hayo leo (Jumatatu, Juni 18, 2018) wakati akifunguaKongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa LAPF, jijini dodoma.
“Pia, huduma za fedha jumuishi ni kigezo ambacho kimeiweka Tanzania mahala pazuri kwenye uchumi jumuishi ambapo zaidi ya Watanzania milioni 30 wamekuwa wakifanya miamala mbalimbali ya fedha kupitia simu za mkononi na hivyo kuongeza huduma za fedha kufikia asilimia 65,” amesema.
Amesema huduma za msingi za kijamii kama vile elimu, afya na kupungua kwa rushwa katika utoaji huduma za umma pamoja namtandao wa miundombinu ya barabara ambayo huwezesha wananchi wengi kujishughulisha na shughuli za kiuchumi ni kigezo kingine kilichozingatiwa katika kuipatia Tanzania nafasi hiyo.
Waziri Mkuu ameongeza kwamba Serikali inaamini kuwa uchumi wa viwanda ukiimarika uchumi utakuwa kwa kasi kubwa na matokeo yake yataonekana wazi kwa kupanua wigo wa ajira, soko la huduma na shughuli nyingine za kiuchumi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kongamano
la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye ukumbi wa LAPF jijini
Dodoma Juni 9 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye
Ulemavu Jenista Mhagama akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa kufungua Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018.
Baadhi
ya washiriki wa Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Kongamano
hilo kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizinduaTaarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa
ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mei 2017 Mpaka Mei 2018 baada ya
kufungua Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika
kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kushoto ni Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha Taarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa
ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mei 2017 Mpaka Mei 2018 baada ya
kuizindua katika Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
lililofanyika kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kushoto
ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mhandisi, Salome Kabunda kutoka
TANROADS Tuzo ya Uwezeshaji Kiuchumi, baada ya TANROADS kuibuka mshindi
wa kwanza katika kundi la Wizara, Wakala na Idara za Serikali kwenye
Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofunguliwa na
Waziri Mkuu katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kulia ni
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John
Jingu.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...