Na Hamza Temba-Arusha

Itifaki ya Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) imezua mjadala mzito na mabishano makali katika Mkutano wa Nane wa Kisekta wa Baraza la Mawaziri wa jumuiya hiyo uliofanyika Jijini Arusha juzi.

Mvutano huo ulisababishwa na hoja iliyowasilishwa na Tanzania ambayo ilitaka kuboreshwa kwa kifungu cha nne cha itifaki hiyo ambacho kinazitaka nchi wanachama kutangaza eneo lote la jumuiya ya Afrika ya Mashariki kama kituo kimoja cha safari za utalii duniani.Tanzania ikiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, ilipinga vikali na hatimaye ikagoma kusaini itifaki hiyo ambayo imejadiliwa kwa zaidi ya miaka saba mpaka pale mapendekezo yake yalipoingizwa kwenye kifungu hicho.

Kifungu hicho kilikuwa kinasema, "Every Partner State shall market and promote the Community as a single tourist destination", (Kila nchi mwanachama itatangaza jumuiya kama kituo kimoja cha safari za utalii (duniani)).Tanzania ikapendekeza kwenye kifungu hicho uongezwe mstari unaosema, "while maintaining country identites" (huku kila nchi mwanachama ikibaki na utambulisho wake halisi).

Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Waziri wa Utalii, Wanyamapori na Mambo ya Kale wa Uganda, Ephraim Kamuntu (katikati) na wawakilishi wa Mawaziri wa Utalii wa Burundi, Kenya na Rwanda wakisaini Itifaki ya Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) katika ukumbi wa EAC Jijini Arusha. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Waziri wa Utalii, Wanyamapori na Mambo ya Kale wa Uganda, Ephraim Kamuntu (katikati) na wawakilishi wa Mawaziri wa Utalii wa Burundi, Kenya na Rwanda wakisaini Itifaki ya Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) katika ukumbi wa EAC Jijini Arusha. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasilisha mapendekezo ya Tanzania kwenye kifungu cha nne cha Itifaki ya Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika Mkutano wa Nane wa Kisekta wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo uliofanyika jijini Arusha. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Dk. Aloyce Nzuki.
Baadhi ya wajumbe wa Tanzania walioshiriki mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...