Na James Ndege
TFDA imeendesha mafunzo ya siku mbili kwa wajasiriamali wadogo wa usindikaji wa vyakula mkoani Tabora ikiwa ni mojawapo ya mikakati yake ya kuwezesha ukuaji wa Sekta ya  viwanda nchini. Mafunzo yamehusisha wajasiriamali 80 wa mkoa wa Tabora   kuanzia tarehe 5 – 6 Juni 2018 katika ukumbi wa Mkutano wa Isike Mwanakiyungi uliopo mjini Tabora.

Akifungua mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bi. Agnes Sitta Kijo aliwaasa washiriki kutumia fursa hiyo kwa ukamilifu ili waweze kukidhi vigezo muhimu vya kisheria na kuzalisha bidhaa bora, salama na zenye ufanisi ili kukidhi soko la ndani na nje ya nchi jambo litakalochangia ukuaji wa uchumi wa nchi lakini pia kulinda afya ya jamii kwa kuwa TFDA ipo karibu na kundi hili muhimu katika uanzishaji wa viwanda nchini kwa kutatua changamoto zao.

“Ili kuwawezesha wajasiriamali wadogo nchini kutatua changamoto zinazowakabili katika usajili wa majengo na bidhaa zao, TFDA ilisainiana hati ya makubaliano (Memorundum of Understanding – MoU) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kupunguza gharama ya usajili zinazowakabili ambapo TFDA itatumia matokeo ya TBS ya vipimo vya maabara katika kusajili bidhaa zao”, alifafanua Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo.

Katika mafunzo hayo, TFDA ilishirikisha Taasisi nyingine za Serikali za Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kuwawezesha wajasiriamali kutambua mambo muhimu yanayotakiwa katika kuzalisha bidhaa zinazokubalika. Mafunzo hayo ni endelevu na Tabora imekuwa mkoa wa 21 nchini kupata mafunzo ya aina hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA. Bi Agnes Sitta Kijo akifurahia jambo kutoka kwa wasindikaji wadogo ya vyakula mkoani Tabora (hawapo pichani) alipofungua mafunzo ya siku mbili kuanzia  tarehe 5 – 6 Juni 2018 katika ukumbi wa Mkutano wa Isike Mwanakiyungi, Tabora.
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA. Bi Agnes Sitta Kijo (aliyekaa katika kiti katikati) akiwa katika picha ya pamoja baina ya Wajasiriamali Wadogo wa Usindikaji wa Vyakula mkoani Tabora, Watumishi wa TFDA, na wawezeshaji kutoka Taasisi za Serikali katika mafunzo ya siku mbili kuanzia tarehe 5 – 6 Juni 2018 katika ukumbi wa Mkutano wa Isike Mwanakiyungi, Tabora

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...