Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mary Majula ( wa sita kushoto) akiiongoza meza kuu kushuhudia magari mawili kati ya 10 yatakayoshindaniwa na wateja wa M-Pesa yaliyotolewa wakati wa hafla ya kutimiza miaka kumi ya M-Pesa iliyofanyika jana Jijini Dsm. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Raymond Mfungahema (wa tano kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao, Mkurugenzi wa kitengo cha M-pesa Ashutosh Tiwary na Mkurugenzi wa Mifumo ya malipo ya Kitaifa wa Benki Kuu Tanzania (BoT) Benard Dodi.
Mgeni rasmi katika sherehe ya miaka 10 ya M-Pesa, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mary Majula (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Mifumo ya malipo ya Kitaifa wa Benki Kuu Tanzania (BoT) Benard Dodi, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Raymond Mfungahema na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao, wakifuatilia moja ya burudani wakati wa sherehe ya kusherehekea mika 10 ya M-PESA iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Moja ya magari mawili kati ya 10 yatakayoshindaniwa na wateja wa M-Pesa yakiwa katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuzinduliwa wakati wa sherehe kusherehekea miaka 10 ya M-pesa .Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya Biashara wa M-Pesa, Polycarp Ndekana na mshereheshaji Taji Liundi.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalyn Mworia (kulia) Mkurugenzi wa kitengo cha M-pesa Ashutosh Tiwary (katikati) na Mkuu wa kitengo cha Mwendelezo wa Biashara ya M-Pesa, Polycarp Ndekana wakiangalia moja ya gari kati ya 10 yatakayoshindaniwa na wateja wa M-pesa wakati wa sherehe ya kusherehekea miaka k10 ya M-pesa iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...