Na Pamela Mollel,Arusha

Vyuo mbalimbali nchini vimetakiwa kuhamasisha wanafunzi wa kike kupenda kusoma masomo ya sayansi kuanzia ngazi za chini ili kuondoa changamoto ya uhaba wa wanasayansi wa kike uliopo hapa nchini. 

Aidha imeelezwa kuwa, kumekuwepo na uhaba mkubwa wa wanasayansi wanawake katika sekta mbalimbali hali inayochangiwa na kuwepo Kwa idadi ndogo ya wanafunzi wa kike wanaohitimu vyuoni. 

Hayo yalisemwa Jana na Mkurugenzi wa ufuatiliaji na udhibiti kutoka baraza la elimu ya ufundi, Dokta Annastella Sigwejo wakati akifungua kongamamno la kiteknolojia lililowashirikisha wanavyuo mbalimbali na makampuni jijini Arusha. Alisema kuwa, ili kuhakikisha tunapata wanasayansi wa kutosha ni lazima tuanze kuhamasisha wanafunzi wakiwa tangu ngazi za chini mashuleni ili wajijengee tabia ya kupenda masomo hayo hadi kufikia ngazi za juu .

Dokta Sigwejo alisema kuwa,kwa sasa hivi ambavyo nchi yetu inahamasisha Tanzania ya viwanda ni lazima kuwepo na wataalamu wanasayansi wa kutosha ambao wataweza kuziba mapengo mbalimbali yaliyopo na hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhamasisha wanavyuo kupenda masomo ya sayansi. 

Kwa upande wa Mkuu wa idara ya Tehama upande wa taalamu kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha, Pamela Chogo alisema kuwa, kongamano hilo ni la kwanza kufanyika jijini Arusha ambapo wameweza kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaosoma masomo ya sayansi jijini hapa pamoja na makampuni ili wajadili changamoto mbalimbali zilizopo .

Alisema kuwa, kumekuwepo na changamoto kubwa ya makampuni mengi kutokupenda na kuzidhamini Kazi zinazozalishwa na wazawa, hivyo kupitia kongamano hilo wanavyuo wataweza kuonyesha Kazi zao Kwa makampuni mbalimbali ili waweze kuzitambua na kuanza kuzitumia. 
Mkurugenzi wa ufuatiliaji na udhibiti kutoka baraza la elimu ya ufundi, Dokta Annastella Sigwejo wakati akifungua kongamamno la kiteknolojia lililowashirikisha wanavyuo mbalimbali na makampuni jijini Arusha,Chuo cha Uhasibu Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel Arusha)
Mkuu wa Idara ya Tehama upande wa taalamu kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha, Pamela Chogo akizungumza na waandishi wa habari , alisema kongamano hilo ni la kwanza kufanyika jijini Arusha ambapo wameweza kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaosoma masomo ya sayansi jijini hapa pamoja na makampuni ili wajadili changamoto mbalimbali zilizopo .
Kaimu Meneja Mamlaka ya Mawasiliano kanda ya Kaskazini Francis Msungu,akizungumza na vyombo vya habari alisema ni vyema watumiaji wa mitandao wakafanya matumizi salama ya kuelimisha na kuhabarisha zaidi
Wadau wa mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...