Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

WAKIMBIZI mkoani Kigoma wametakiwa kurejea nchini kwao, ili waanze kujishughulisha na masuala ya maendeleo kwani kwa sasa nchi zao ziko salama na amani imerejea.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala katika kambi ya Mtendeli wakati wa Siku ya Wakimbikiz Duniani.

Amesema sasa ni wakati wa wakimbizi waliko chini kurudi katika nchi zao kuendelea na majukumu mengine.Amefafanua mkapa sasa baadhi ya wakimbizi 6000 wamerejea nchini mwao kwa hiyari. "Wapo wengine bado wapo nchini kwetu kutokana na kushawishiwa na baadhi ya watu kwa maslahi yao binafsi,"amesema.

Amewaambia wakimbizi hao ni vema wakarejea nchini kwao na kuendelea na maisha yao badala ya kubaki Tanzania kwasababu kuna watu wanawashawishi.Aidha amesema Serikali haitawavumilia wakimbizi wanaoishi katika kambi zilizopo wilayani hapo ambao watabainika kujihusisha na vitendo vya kiualifu.

"Serikali imewahakikishia kuishi kwa amani na usalama wao pamoja na mali katika kambi yao na sambamba na kuilinda amani hiyo ambayo waliikuta nchini," amesema Ndagala Amefafanua kila mkimbizi anatakiwa kufata taratibu na sheria za nchi na kwa kila atakayekiuka taratibu hizo sheria haitamuacha salama lazima itafata mkondo wake.Pia amesema kuna changamoto ya uhalifu, kwani kuna baadhi ya wakimbizi wamekuwa wakitoka kambini na kwekuharibu mazao katika mashamba ya watanzania.

Awali akisoma hotuba Mwenyekiti wa kambi hiyo Mtena Nizigiyumukiza ameiomba Serikali ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi(UNHCR), kufanya mahojiano na wakimbizi ambao hawako tayari kurudi nchini kwako ili wasikilizwe matatizo yao. "Tunaomba pia mtuongezee sabuni pamoja na chakula ikiwa sambamba na kubadilishiwa chakula kwani tumekuwa tukila ugali na imetufanya kutamani wali,"amesema Nizigiyumukiza.

Mkuu wa kambi hiyo Lulu Malima, amewataka wakimbizi hao kutunza mazingira ndani na nje ya kambi na kuacha tabia ya kukata miti ovyo.
Baadhi ya Wakimbizi wa kambi ya Mtendeli iliyopo wilayani Kakonko Mkoani Kigoma wakiadhimisha  katika siku ya wakimbizi duniani,
 Shughuli za burudani hapa na pale zilitolewa katika maadhimisho hayo hapo jana
 Baadhi ya Wakimbizi wa kambi ya Mtendeli iliyopo wilayani Kakonko Mkoani Kigoma wakiadhimisha  katika siku ya wakimbizi duniani,
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...