WAKINA mama 925,342 nchini wamefanikiwa kusajiliwa na mradi wa “Tumaini
la Mama tokea ulipoanza mwaka 2012 na kuweza kunufaika huduma
zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya Mbaruku Mgawa wakati wa kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa
mradi wa “Tumaini la mama kwa viongozi na watendaji mkoani Tanga
kilichofanyika mjini Korogwe.
Alisema idadi hiyo ni kuanzia mpango huo ulipoanza hadi mwezi Mei mwaka
huu huku wakina mama wapatao 323,797 wakitokea mkoani Tanga pekee ambao
wamesajiliwa.
Aidha alisema pia kaya 323.797 zimenufaika na kulipiwa fedha kwa ajili
ya kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambapo sh.milioni
48,077,859,434 zimelipwa kwa watoa tokea mradi huo ulipoanza huku vituo
vya mkoa wa Tanga vikilipwa kiasi cha sh.milioni 12,449,902,412.
“Pia vifaa tiba vyenye ya sh. milioni 900 vimenunuliwa na kusambazwa
katika vituo vya kutolea huduma pia mradi umesaidia upatikanaji wa
computers katika vituo vyenye mahitaji kwa ajili ya kusaidia utunzaji wa
kumbukumbu”Alisema.
“Kwa kuzingatia mafanikio yaliyopatikana mfuko utakaa na mfadhili kuona
uwezekano wa kupata fedha zaidi kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma kwa
wananchi sisi viongozi tunalo jukumu la kuhakikisha kwamba mradi
unatekelezwa kama ilivyokusudiwa ili mfadhili aone umuhimu wa kuongeza
muda zaidi”Alisema.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...