MKUU wa wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza, Bw. Juma Sweda amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanatumia vizuri fedha wanazozipata kutokana na mauzo ya zao la pamba.
Amesema ni vema wakatumia fedha hizo kwa ajili ya kujiletea maendeleo katika familia zao ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba bora na za kisasa na wawaendelea watoto kielimu.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Juni 11, 2018) wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua shughuli za uvunaji na uuzaji wa zao la pamba. Ziara hiyo imefanyika kwenye vijiji vitatu vya kata ya Mondo wilayani hapa.
Bw. Sweda amesema wananchi wengi walihamasika kulima zao la pamba baada ya Serikali kuhamasisha walime na kuahidi kulifuatilia kuanzia hatua za utayarishaji wa mashamba hadi utafutaji wa masoko.
“Naishukuru Serikali kwani baada ya kuhamasisha ufufuaji wa kilimo cha zao la pamba nasi tuliungana na wananchi kuhakikisha maelekezo hayo tunayatekeleza kwa vitendo, lengo letu kubwa ni kuona zao hilo linarudi kama zamani,” amesema.
Amesema kwa sasa wapo katika hatua ya uvunaji na uuzaji, ambapo wamejipanga kukagua kikamilifu ili kuona zoezi hilo linaenda vizuri na pamba yote inayopokelewa na vyama vya Ushirika ni ile iliyo katika ubora unaohitajika.
Amesema viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) hukagua pamba kabla ya kuipokea na iwapo mkulima atabainika kupeleka pamba chafu hulazimika kuisafisha kwanza kwa kutenga safi na chafu ndipo hupima na kulipwa.
Mkuu
wa wilaya ya Misungwi, Juma Sweda (kushoto) akikagua shamba la pamba la
Bw. Swalala Nteminyanda (kulia) katika kijiji cha Nyanh'onge wilayani
humo Juni 11, 2018. Ununuzi wa pamba kwa pesa taslimu wilayani
Misungwi unaendelea vizuri na kilo moja inanunuliwa kwa shillings
1100/=. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkulima
wa pamba katika kijiji cha Mondo wilayani Misungwi, Hoja Ngole
akitumia mkokoteni wa kokotwa na ng’ombe kupeleka pamba yake kuuza
kwenye Chama cha Ushirika wa Mwaniko katika kijiji cha Mondo Juni 11,
2018. Uuzaji wa pamba wilayani Misungwi unaendelea vizuri na kilo moja
inauzwa kwa sh. 1100/=.
Katibu wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Mwanimo, Philip Makoye
akionyesha pamba cha aliyoikataa na kuamuru ichambuliwe tena na mkulima
aliyetaka kuiuza katika chama hecho wilayani Misungwi, Juni 11, 2018.
Wakulima
wa zao la pamba Bibi Pendo Kitwala (katikati) na Sospeter Shija
wakichambua pamba iliyokataliwa baada ya kugundulika kuwa ni chafu
wakati walipotaka kuiuzwa katika Chama cha Ushirika cha Msingi cha
Mwanimo wilayani Misungwi Juni 11, 2011. Ukaguzi wa hali ya juu
unafanyika msimu huu wa uuzaji zao hilo ili kuwanasa wakulima wachache
wanaojaribu kuuza pamba chafu. Lengo la hatua hiyo ni kurejesha
heshima ya ubora na sifa nzuri ya pamba ya Tanzania katika soko la
dunia. Kushoto ni Mussa Daudi akiwasaidia wazee hao.
Katibu
wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Mwanimo, Phillip Makoye (kushoto)
akipima katika mzani pamba ya Marco Masalamunda (watatu kulia) kwenye
ghala la chama hicho cha msingi lililopo Katika jijini cha Mondo
wilayani Misungwi Juni 11, 2018. Ununuzi wa zao la pamba kwa fedha
taslimu unaendelea vizuri wilayani humo na kilo moja inanauliwa kwa
shillingi 1100/=.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...