Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  John Pombe Magufuli kwa ujenzi wa vituo  vya afya 208 vilivyojengwa na Seriakli kwa ajili ya kutoa huduma bora za afya nchini.

Wameyasema hayo mbele ya Kamati ya ufuatiliaji wa ukarabati wa vituo vya afya nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iliyofika katika kituo cha afya cha Mlali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kukagua  maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho kilichopatiwa shilingi bilioni 400 kwa ajili ya ujenzi huo.

Wananchi hao wamesema Serikali imetambua shida za wananchi wa hali chini na kuona umuhimu wa kujenga vituo vya afya nchini  kwa lengo la kupunguza kero za utoaaji wa huduma bora kwa jamii maskini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kituo cha afya Mlali,kilichopo katika  Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Bw. Abbas Mkomwa  ameishukuru Serikali kwa kutoa shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kimeweza kujenga , Nyumba ya Mtumishi, Wodi ya wazazi, Maabara,  Jengo la upasuaji na jengo la kuhifadhia maiti.

Amesema huduma kama hizi zimekuwa zikifanyika lakini kwa sasa jamii imeweza kushirikishwa katika kila hatua za awali za ujenzi wa vituo vya afya hivyo kuweka uwazi kwa jamii na kuona kuwa nao wanawajibu wa kushiriki katika ujenzi wa miundombinu ya vituo vya afya nchini.

“Kwa mara ya kwanza Serikali imeweza kushirikisha wananchi katika shughuli za maendeleo, hii inaonyesha jinsi serikali ya awamu ya tano inavyojdhamini mchango wa wananchi katika kuleta maendeleo“ AmesemaBw. Mkomwa.
 Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Dkt.James Kiologwe  akifafanua jambo kwa Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Mlali leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya afya kuona maendeleo ya ujenzi, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma
Timu ya Dodoma wakikagua miundombinu      ya Kituo cha afya cha Mlali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Jijini Dodoma leo wakati  wakikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...