Na EmanuelMadafa,Mbeya.
Imeelezwa kuwa watu wapatao milioni 270 wanahusika na ajali za kemikali maeneo ya kazi na watu milioni 160 wanasumbuliwa na magonjwa yanayotokana na madhara ya kemikali Duniani .
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali, Christopher Anyango, kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kuelimisha wadau wa madini, wakiwemo wachimbaji, wachenjuaji pamoja na wasambazaji wa vifaa vya kemikali Wilayani Chunya, Mkoani Mbeya.
Amesema, kati yao watu milioni 125 duniani, wako katika hatari ya kudhurika na kemikali aina ya ‘asbestos” huku 90,000 wakipoteza maisha kila mwaka na kwamba madini hayo yanatumiwa zaidi kwenye viwanda vya kutengenezea mabati.
Aidha Mkurugenzi huyo amedai kuwa ukiachana na shughuli za kwenye madini, pia kemikali hiyo ya “asbestos” hutumika kutengenezea mabati na watu wanatumia bidhaa hii kwenye ujenzi wa nyumba hivyo ni vema watengenezaji wa vifaa hivyo wakapatiwa elimu jinsi ya njia bora ya kutumia kemikali hii ili isilete madhara kwa binadamu.
Hata hivyo , amesema kwenye madini mbalimbali kemikali zinazotumiwa ni Sodium Cyanide na Sulphuric Acid na nyinginezo ambazo zote ni hatari kwa afya na mazingira na pia ni kemikali bashirifu hivyo matumizi yake na usimamizi unahitaji uelewa unaojitosheleza ili kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akifungua mafunzo hayo, amewataka wakemia wanahusika na upimaji wa sampuli za madini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa waledi kwa lengo la kuwasaidia wananchi eza kupata dhahabu sanjali na kusaidia kupatikana kwa mrahaba wa serikali.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali, Christopher Anyango, akisoma hotuba kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kuelimisha wadau wa madini, wakiwemo wachimbaji, wachenjuaji pamoja na wasambazaji wa vifaa vya kemikali Wilayani Chunya, Mkoani Mbeya.
Wadau wa madini, wakiwemo wachimbaji, wachenjuaji pamoja na wasambazaji wa vifaa vya kemikali wakiwa makini katika ufunguzi wa semina iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika ukumbi wa mikutano wa Wilayani Chunya, Mkoani Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akifungua mafunzo kwa wadau wa madini, wakiwemo wachimbaji, wachenjuaji pamoja na wasambazaji wa vifaa vya kemikali Wilayani Chunya, Mkoani Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa (katikati ) na viongozi kutoka ofisi ya mkemia walioketi katika picha ya pamoja na wadau wa madini, wakiwemo wachimbaji, wachenjuaji pamoja na wasambazaji wa vifaa vya kemikali Wilayani Chunya katika picha ya pamoja.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...