Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Fainali ya Mashindano ya Kimataifa ya kuhifadhi Quran yanayotarajiwa kufanyika Juni 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo mataifa zaidi ya 20 yameshiriki.

Mashindano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania.Mbali ya kuwepo kwa Waziri Mkuu Majaliwa viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwamo wastaafu nao watakuwa miongoni mwa watakaohudhuria kushuhudia mashindano hayo yenye hadhi ya kimataifa.

Viongozi wastaafu watakaohudhuria siku hiyo ni Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mzee Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne mzee Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais mstaafu Dk.Mohammed Ghalib Bilal pamoja na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mratibu wa Mashindano hayo kutoka Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania Sheikh Mohamed Nasoro amesema tayari washiriki karibu wote wamewasili chini Tanzania ambapo waliopo sasa ni washiriki kutoka mataifa 18 kati ya mataifa 20 ambayo yamealikwa.

Mratibu wa Jumuiya ya Kuhifadhi Qur an Tanzania, Shekh Mohammed Nassor (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mashindano ya kuhifadhi Qur an Kimataifa yanayotarajia kufayika kesho katika ukumbi wa Diamond Jubilee June 3, 2018. Kulia ni Katibu wa Jumuiya hiyo, Shekh. Mohamed Ali Hassan na Jaji wa mashindano hayo, Dk. Abbas Hamza Mohammad.

Katibu wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania Sheikh Mohamed Ali Hassan(kulia) akielezea kwa kina kuhusu mashindano hao yanayotarajia kufanyika Juni 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa majaji kutoka nchini Somalia (wa pili kushoto) akizungumzia namna ambavyo wamejiandaa kuchuja washiriki kwenye mashindano hayo.Wa kwanza kulia ni Katibu wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania Sheikh Mohamed Ali Hassan na anayefuatia ni Mratibu wa mashindano hayo Sheikh Mohamed Nasoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...