Na Anthony Ishengoma Singida.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezindua mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake vijana leo Mkoani Singida kwa lengo la kuutambulisha kwa jamii kuhusu wasichana na wanawake vijana walio shuleni na walio nje mfumo wa Elimu.
Mradi huu unatekelezwa na Wizara pamoja na wadau wa Maendeleo kutoka AMREF, TAYOA, TASAF, TACAIDS na Mfuko wa Kimataifa wa Global Fund na wakati huu mradi uko katika hatua ya majaribio katika mikoa mitatu ya Tanzania ambayo ni Singida, Dodoma na Morogoro.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa mradi huu mapema leo mjini Singida Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Marcel Katemba amesema kimsingi Wizara yake imepewa jukumu la kuandaa mazingira rafiki na wezeshi ya utekelezaji wa Mradi huu na ndiyo maana hatua ya awali ya maandalizi inaanzia kwa kujenga uwezo kwa wataalamu wa maendeleo ya Jamii kutoka mikoa ya majaribio ya mradi.
Aidha Bw. Katemba amesema Serikali ya Tanzania imepata ruzuku kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Global Fund kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali ya mapambano dhidi ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Nchini kwa kipindi cha January 2018 mpaka Desemba 2020.
Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Marcel Katemba akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mradi
wa kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake
vijana leo Mkoani Singida.
Mkurugenzi
wa Idara ya watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Margaret Mussai akizungumza na wajumbe wa Mkutano
wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa
wasichana balehe na wanawake vijana leo Mkoani Singida.
Naibu
Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu akitoa neno la shukrani kwa
viongozi wa Wizara hawako pichani wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia
maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake vijana leo
Mkoani Singida.
Uongozi
wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja
na Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Singida, Taasisi za TASAF na
TACAIDS na wadau wa maendeleo kutoka Amref na TAYOA wakiwa katika picha
ya pamoja wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU na
Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake vijana leo Mkoani Singida. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...