Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MBUNGE wa Mkuranga na Naibu Waziri Ufugaji na Uvuvi Abdallah Ulega ameendelea na ziara yake katika jimbo la Mkuranga katika kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi wa jimbo hilo.
Akizungumza na wananchi wa jimbo hilo Ulega amesisitiza umoja na mshikamano katika kuleta maendeleo katika jimbo hilo kwa mustakabali wa kizazi kijacho na amesema anatambua changamoto ambazo bado zinazikabili jimbo lao na ataendelea kupambana nazo.
Ulega amefafanua kuwa kuhusu maeneo yenye changamoto kama miundombinu ya barabara kukatika baada ya mvua kupita tayari fedha zimetengwa kwa maeneo hayo na kinachosubiriwa ni utekelezaji wa makandarasi.
Ulega amesisitiza kuwa ataendelea na jitihada zake na kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kupunguza kama si kumaliza kero ambazo bado zipo katika baadhi ya maeneo hasa katika elimu, afya na masuala ya kijamii.
Mkazi wa Mkuranga Yasin Ligwema ameeleza kuwa vyoo vipewe vipaumbele katika shule ili kuwaweka wanafunzi hasa watoto wa kike katika kujisitiri.
Aidha wananchi wamempongeza Mbunge wao katika kutoa vipaumbele katika masuala ya maji, elimu na afya.
Ulega alihitimisha ziara hiyo kukabidhi zakatulfitry kwa wajumbe waliohudhuria.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega na akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Mlamleni katika mkutano huo.
Sehemu ya wanachi wa kijiji cha Mlamleni wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi, Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega katika mkutano huo.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mlamleni juu ya kuendelea kushirikiana na wanachi kwa kila jambo na kutatua kero zao.(picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
Mmoja wa wazee wa kijiji cha Mlamleni akielezea kero yake mbele ya Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...