Kauli ya Naibu Waziri huyo aliitoa juzi wakati wa ziara yake ya kutembelea Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto alipokuwa akikagua miradi ya maji huku akilazimika tena kumsimamisha kazi Mhandisi wa Maji Samadu Makau kutokana na kushindwa kusimamia vema mradi wa Maji Mgwashi wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 1.5 na kupelekea wananchi kukosa maji.
Naibu Waziri ambaye alianza ziara yake mkoani Tanga kwenye wilaya ya Handeni,Korogwe,Lushoto na Halamshauri zote ndani ya wilaya hizo ambapo alibaini kuwepo kwa ubadhirifu mkubwa wa fedha za serikali katika miradi ya maji tokea mwaka 2012 kutokana na kutokuwepo kwa usimamizi makini wa watendaji wa serikali.
Alisema ubadhirifu na upotevu wa fedha za Serikali inatokana na wahandisi wa maji wa mikoa na wilaya waliopewa jukumu la kusimamia miradi hiyo na kushauri kushindwa kuwajibika ipasavyo hivyo kupelekea kuingiza hasara na kupelekea wananchi kukosa maji hivyo Wizara kuanza kutilia mashaka taaluma zao.
Naibu Waziri huyo alisema haiwezekani serikali inapeleka fedha nyingi kwenye miradi ili kuweza kutatua tatizo la uhaba wa maji kwa wananchi huku wahandisi hao wa maji wakishindwa kusimamia kwa waledi miradi hiyo huku Serikali ikiwalipa fedha za mishahara kwa ajili ya kuisadia majukumu hayo.
“Haiwezekani Serikali inatumia fedha nyingi sana kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kwa lengo la kuondokana na adha hiyo huku wahandisi waliopo kwa niaba ya Serikali wakishindwa kuisimamia badala yake unapewa taarifa ya ubabaishaji kila maeneo ya miradi unapotembelea”Alisema.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akionyeshwa na wananchi wa Kijiji cha Manolo Kata ya Manolo wilayani Lushoto maji wanayotumia kutoikana na kukabiliana na uhaba wa maji wakati wa ziara yake juzi iliyokuwa na lengo la kukagua miradi ya maji na kuzungumza na wananchi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...