BALOZI wa Korea Kusini, Mh. Geum-Young Song amesema kwamba atasaidia haja ya uwekezaji wa uunganishaji magari nchini Tanzania pamoja na kuiwezesha Tanzania kuwa kitovu cha tehama kwa nchi za Kusini, Kati na Mashariki ya Afrika.
Alisema hayo kwenye mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Katika mazungumzo hayo Balozi huyo wa Korea Kusini alisema kwamba atahakikisha anafanya kila kinachowezekana kushawishi makampuni ya magari ya Korea kusini kuanza kuunganisha magari hayo nchini Tanzania.
Dk. Mengi katika mazungumzo hayo alisisitiza haja ya kuanza mazungumzo ya kina ya ushirikiano katika kuunganisha magari kabla ya kuingia katika masuala ya simu zenye utendaji wa kisasa (Smart Phones) na tehama kwa ujumla.
Alisema pamoja na kukubaliana na wazo la Dk. Mengi kuhusu haja ya kuwa na kampuni ya kuunganisha magari nchini Tanzania katika kuelekea uchumi wa viwanda taifa kutengeneza magari yake yenyewe, alisema kama taifa wana mpango wa kusaidia Tanzania kuwa taifa la viwanda likiongoza katika tehama.
Alisema kwa kuwa taarifa na mambo mengi ya habari ndio nguvu kwa vijana kuelekea katika ustawi wangelipenda kuwa na eneo ambalo vijana watalitumia katika kupata maarifa na kuyatumia kuboresha hali zao na kukua kiuchumi.
Katika mazungumzo hayo Dk. Mengi alisema kwamba kuwapo na viwanda vya magari nchini Tanzania ni ndoto yake na kwamba alikuwa amepanga kwenda Sri Lanka kushawishi ushirika katika uunganishaji magari kuelekea kuyatengeneza Tanzania.
Mwenyekiti
Mtendaji wa IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi akizungumza na Balozi wa Korea
Kusini nchini, Geum-Young Song wakati Balozi huyo alipomtembelea ofisini
kwake jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa
Biashara na Uwekezaji wa Korea, Hong Kyun Lee. Balozi wa Korea, Dk Mengi wazungumzia uunganishaji magari ya Korea nchini Tanzania.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...