Bodi
ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) inayoongozwa na Mwenyekiti Prof. John
Kondoro imeshiriki mafunzo ya siku mbili ya uongozi kwa wajumbe wa Bodi
(Board Leadership Training) yalioandaliwa na Menejimenti ya shirika la
Reli na kuratibiwa na Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (Institute of
Directors in Tanzania) kuanzia tarehe 2 - 3 Juni katika ukumbi wa Bodi,
jengo la LAPF jijini Dodoma.
Lengo la kuandaa mafunzo ni kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi katika shughuli za uendeshaji wa Shirika. Bodi ya Shirika la Reli Tanzania imeundwa na wajumbe nane (8) wenye ujuzi mbalimbali kwa kufuata sheria mpya ya Reli namba 10 ya Mwaka 2017. Bodi ya Shirika la Reli ilizinduliwa rasmi tarehe 11 mwezi Juni 2018 na aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.
Wajumbe.
1. Prof. John Kondoro-Mwenyekiti
2. Eng. Karim Mattaka-Mjumbe
3. Dkt. Jabiri Bakari-Mjumbe
4. Masanja Kadogosa-Katibu wa bodi
5. Eng. Rogers Mativila
6. Rukia Shamte-Mjumbe
7. Edson Mweyunge-Mjumbe
8. Wolfgang Ephraim Salia-Mjumbe 9. MahamudMabuyu-Mjumbe

Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kadogosa akitoa mfano alipokuwa akifafanua jambo walilokuwa wakijadili katika mafunzo ya wajumbe wa Bodi mpya ya TRC yaliyofanyika jijini Dodoma, tarehe 2 Juni 2018.
Katibu wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Ndg. Masanja Kadogosa akiwakaribisha wajumbe wa Bodi mpya ya TRC wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na menejimenti ya TRC.
Mjumbe wa Bodi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (wa kwanza kulia) Eng. Mattaka akielezea jambo kwa kina huku mwenyekiti Prof. Kondoro na mwezeshaji Ndugu Said Kambi wakifuatilia kwa makini.

Dr. Jabiri Bakari (katikati) akielezea jambo kwa msisitizo wakati wa mafunzo ya wajumbe wa Bodi ya TRC yaliyoandaliwa na menejimenti ya Shirika la Reli Tanzania na kufanyika jijini Dodoma.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa Bodi mpya ya Shirika la Reli Tanzania, waratibu kutoka Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania na Sektretarieti ya Shirika la Reli Tanzania katika jengo la LAPF jijini Dodoma.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...