Na Emmanuel Madafa,
Globu ya Jamii, Mbeya
Watu watano wanadaiwa kufariki dunia usiku katika ajali iliyohusisha lori pamoja na gari dogo aina ya Noah eneo la mteremko wa mlima Igawilo nje kidogo ya jiji la Mbeya.
Globu ya Jamii, Mbeya
Watu watano wanadaiwa kufariki dunia usiku katika ajali iliyohusisha lori pamoja na gari dogo aina ya Noah eneo la mteremko wa mlima Igawilo nje kidogo ya jiji la Mbeya.
Mwandishi wa Globu ya Jamii ambaye yuko eneo la tukio hivi sasa ameambiwa na mashuhuda wa tukio hilo kwamba huenda chanzo cha ajali hiyo ni lori ambalo liliferi breki na kuzigonga gari nyingine tatu zikiwemo za TANESCO na kampuni ya CocaCola pamoja na hiyo Noah ambayo ilikuwa na abiria watatu ambao wawili inahofiwa wamefariki papo hapo na mmoja amekimbizwa hospitali rufaa ya Mbeya kupatiwa matibabu.
Dereva wa lori na msaidizi wake wanahofiwa kwamba wamefariki dunia papo hapo na juhudi za kuondoa maiti zao zimekuwa zikiendelea wakati wa kutuma taarifa hii.
Ajali hii imekuja masaa machache tu baada ya waziri mpya wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola kumaliza ziara yake mkoani Mbeya ambapo pamoja na mambo mengine amevunja kamati na mabaraza ya usalama barabarani nchi nzima kwa nia ya kujipanga upya katika kupambana na janga hilo sugu la Taifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...