Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MBUNGE wa Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam Mwita Waitara kupitia Chadema ametangaza rasmi kujiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Ametangaza uamuzi huo leo katika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam ambapo kabla ya Waitara kuzungunza Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole alitangaza kuwa wanapokea mtu muhimu.
Akizungumza wakati anatangaza huo amesema ameamua kurudi CCM kwasababu lengo lake ni kusaidia wananchi wa Ukonga jijini Dar es Salaam na kufafanua kuna mambo anashindwa kufanya kutokana na kukwamishwa na viongozi wa ngazi za juu wa Chadema.
Amefafanua kila anapotaka kuzungumza na viongozi wa Serikali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Ukonga viongozi wa Chadema wanamzuia asizungumze na mawaziri kisa wapo CCM. Amesema kwa mazingira hayo ameona ni bora akahamia upande wa pili ambao ni wa CCM na kufafanua kuwa anajua Watanzania watashituka lakini anaomba wamuelewe kwani nia yake ni njema.
Amesema amesema Chadema inajinasibu kuwa ni chama cha demokrasia lakini ukweli ni kwamba hakuna semokrasia na hivyo kuanzia sasa si mbunge wa Chadema.Pia ametangaza kujivua nafasi zote ikiwamo ya Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Pwani na kuongeza pia si Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam. Amesema amesema anataka kuwa huru kwani amechoka kukaa maisha ya kutokuwa huru na kuongeza kwa sasa anaangalia namna bora ya kuendelea kuwatumikia wananci.
",Haya ni maamuzi yangu binafsi,nimetafakari vya kutosha.Nimekaa katika chama cha maigizo na pale Chadema ni sanaa tu.
" Nimepata baraka za wazee wangu wa kabila la Wakurya,hivyo niko salama na kwamba wananchi wanaohitaji maendeleo lazima waunge mkono juhudi za serikali,"asema Waitara.

Amefafanua kuingia kwake CCM haina maana amenunuliwa bali ni uamuzi wake na kueleza Rais Dk.John Magufuli anafanya kazo nzuri ambayo inastahili kuungwa mkono na Watanzania wote. Amesema kuwa Rais Magufuli amefanikisha kuziba mianya ya rushwa na ameimarisha ukusanyaji wa kodi.
Hivyo amesema kuna mambo mengi ambayo yamemuondoa chadema na hayupo tayari kibaki Chadema kwani hataki kufa kwa ugonjwa wa moyo. Ametumia nafasi hiyo kueleza ugomvi wake na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe umetokana na uchaguzi ndani ya chama hicho.
Amesema baada ya kuhoji kumuuliza Mbowe amekaa muda mrefu hapo ndipo tatizo lilipoanzia na amedai kutishiwa maisha hovyo ameona ni bora akaa kando. Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa suala la uenyekiti Chadema si la Waitara peke yake bali kuna wabunge wengi wa Chadema wanataka mabadiliko.
Amesema kuna wabunge wengi wanataka Mbowe aondoke na wamejipanga kumng'oa maana wanachotaka ni mabadiliko na kusisitiza Mbowe ameshamtikia kauli za vitisho. Amesema anakumbuka Chacha Wangwe alipotaka kugombea uenyekiti wa Chadema alishughulikiwa na leo hayupo,hivyo naye anaogopa yasimkute ya Wangwe.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteeeeh! hapa kazi tuu! na watajiunga wengi aisee! kwa wale wanaotafuta ajira tembele hapa kupata ajira inayokufaa https://www.ajiriwa.net
ReplyDelete