Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewasili mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi na Julai 5 mwaka huu anatarajiwa kufunga mafunzo katika Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza ambayo yana lengo la kukabiliana na uhalifu unaotokea katika Bahari, Maziwa na Mito hapa nchini.
Pamoja na ufungaji wa mafunzo hayo pia ataendelea na ziara ya kukagua utendaji wa Polisi katika baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kuhakikisha uhalifu unapungua  hapa nchini ikiwemo ajali za barabarani, Maujai ya kishirikina na uhalifu katika Visiwa vilivyopo Ziwa Viktoria.


Katika ziara hiyo ya kikazi atakagua utendaji wa Polisi katika baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kuhakikisha uhalifu unapungua  hapa nchini ikiwemo ajali za barabarani.
Baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza IGP Sirro amepokelewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi na kufanya kikao na Maofisa waliopo katika Mkoa huo nakuwataka kuwajibika ipasavyo kuzuia ajali za barabarani kama ilivyo kwa makosa mengine.
“Nimekuja kukagua utendaji wenu ili kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili ili kufikia malengo tuliyojiwekea ya kuhakikisha uhalifu unapungua hapa nchini, hivyo ni imani yangu kila mmoja atawajibika kwa nafasi yake na kuwasimamia waliopo chini yake ipasavyo” Alisema IGP Sirro
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ahmed Msangi amesema hali ya usalama katika mkoa huo ni shwari na suala la usalama barabarani linaendelea kusimamiwa kikamilifu kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine zinazohusika.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya kikazi  kwenye baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ahmed Msangi (Kulia) na Afisa Mnadhimu wa Mkoa huo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Advera Bulimba (Kulia) baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya kikazi kwenye baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akipokea Salam ya heshima baada ya kuwasili Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Mwanza kwa ziara ya kikazi katika baadhi ya mikao ya Kanda ya Ziwa.Kushoto ni Kamanda wa mkoa huo, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ahmed Msangi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimfariji Bi Lily Matola ambaye ni Afisa Mnadhimu Mstaafu wa Polisi mkoani Mwanza baada ya kufiwa na Mume wake Marehemu Edmund Matola. IGP Sirro yupo ziara ya kikazi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kuangalia utendaji wa Polisi hususani katika kupunguza ajali za barabarani nchini.
Habari na Picha na Jeshi la Polisi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...