Na Geofrey Chambua
kutoka vyanzo mbalimbali
Ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner ni ya ukubwa wa wastani, yenye injini mbili inayotengenezwa na kampuni ya Boeing ya Marekani.
Kwa mara ya kwanza ndege hii ilirushwa mnamo mwaka 2009 na ilikua ipewe jina la 7E7 (E Ikimaanisha Efficiency-Ufanisi) lakini ikabadilishwa na kuitwa 787 Ili kuendana na mazoea ya ;majina ya ndege a aina hiyo.
Matumizi yake ya mafuta ni wa asilimia 20 chini cha ndege ya ukubwa sawa na huo na ndiyo ndege ya Boeing inayotumia kiwango cha chini zaidi cha mafuta.
Injini zake zimejengwa kwa njia maalumu ili kupunguza sauti ndani na pia nje ya ndege kwa hadi asilimia 60. Madirisha yake ni makubwa kuliko ya ndege zingine za ukubwa kama huo kwa asilimia 65 (47 by 28 centimeters)
Kinyume na mfumo unaotumiwa kawaida wa kufungua kuongeza au kupunguza mwangaza wa dirisha kwenye ndege, kwa ndege hii ni kibonyezo ambacho hutumika kwa kutumia teknolojia ya kabadilisha rangi ya kioo kukiwezesha kudhibiti mwangaza unaoingia.
Ina uwezo wa kubeba hadi abiria 262 ikiwa pia na uwezo wa kusafiri umbali wa kilomita 13,621 bila kusimama.
Boeing 787-8 ilijengwa kuchukua mahala pa ndege aina za 67-200ER na 300ER.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...