Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo amewaagiza wataalam wa sekta ya afya wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kutunza vifaa tiba vilivyotolewa kwa msaada kutoka Taasisi ya Dhi Nurein Foundation.

Taasisi hiyo imesaidia ujenzi wa jengo la dharula, wodi ya wazazi, pamoja na vifaa mbalimbali vya afya ambapo Mradi huo umegharimu zaidi ya Sh.Milioni 900. Hatua hiyo ya taasisi hiyo ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa wilaya ya Bagamoyo na maeneo mengine hapa nchini. 

Akizungumza katika uzinduzi wa Mradi huo kwa niaba ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Jafo amesema taasisi hiyo inaungana na taasisi zingine hapa nchini zinazosaidia miradi mbalimbali na kuagiza vifaa hivyo kulindwa na kutunzwa bila kupoteza. 

Jafo amesema kuna baadhi ya watu wachache hapa nchini wasio waadilifu wamekuwa na tabia ya kuchukua vifaa vizuri vya hospitali na kuvihamishia katika hospitali zao binafsi. Wakati huo huo, Waziri Jafo amewapongeza sana Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, pamoja na Mbunge wa Bagamoyo Shukuru Kawambwa kwa kufanikisha upatikanaji wa mradi huo.

Pia Jafo amewaomba wananchi wajiunge katika mifuko mbalimbali ya bima ya afya ikiwemu CHF iliyo boreshwa ili waweze kupata huduma bora ya matibabu wao na familia zao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiongea na wananchi wa Bagamoyo
Dkt. Saleh kutoka nchini Saudia kutoka taasisi iliyofadhili mradi huo akitoa maelezo ya mradi kwa Waziri wa Tamisemi Mhe. Selemani Jafo.
Wananchi wa Bagamoyo wakiwa katika mkutano wa uzinduzi wa Mradi wa afya ya mama na mtoto katika hospitali ya wilaya ya Bagamoyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja mjini Bagamoyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...