WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa mkoa wa Simiyu na halmashauri zake kwa kusimamia vyema ujenzi wa miradi ya afya mkoani humo. 

Jafo ametoa pongezi hizo wakati akipokea vituo vya afya 38, magari ya wagonjwa matatu, magari ya kuratibu shughuli za afya sita , pamoja na vifaa vilivyofadhiliwa na shirika la Kimataifa la UNFPA wakishirikiana na KOICA. Katika makabidhiano hayo,Waziri Jafo amefurahishwa na usimamizi mzuri wa ujenzi wa miundombinu hiyo kupitia utaratibu wa FORCE ACCOUNT. 

Jafo amempongeza mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka pamoja na wabunge wa mkoa huo kwa kuwashirikisha vyema wananchi ambao wameungana na serikali yao pamoja na wadau katika kufanikisha miradi hiyo ya afya. Katika shughuli hiyo waziri Jafo amesisitiza magari hayo tisa yatumike kwaajili ya sekta ya afya na si vinginevyo. 

Wakati huo huo, Waziri Jafo amefurahishwa na wananchi wa Malya wilayani Kwimba mkoa Mwanza kwa kujenga vizuri sana majengo yao ya kituo cha afya Malya baada ya serikali kuwapatia fedha milioni 400.

Naye mbunge wa Sumve Mhe. Ndasa aliishukuru serikali na ameiomba kuwasaidia mashine ya X-Ray kituoni hapo ili wananchi waondokane na usumbufu wa kwenda hospitali ya wilaya iliyopo Ngudu.Waziri Jafo amemaliza ziara yake ya mikoa miwili ya Simiyu na Mwanza na kuelekea wilayani Bagamoyo kwaajili ya uzinduzi wa jengo la wazazi katika hospitali ya wilaya ya Bagamoyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akisikiliza maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Baadhi ya vifaa vilivyopo kwenye vituo vya afya vya mkoa huo vilivyozinduliwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Sumve Richard Ndassa katika uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Afya Malya wilayani Kwimba mkoa Mwanza.

Majengo yaliyojengwa kwa ufadhili wa shirika la UNFPA na KOICA.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akikagua ujenzi unaoendelea katika Kituo cha Afya Malya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...