Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage, akizungumza wakati wa kikao na Uongozi wa Benki ya CRDB, walipotembelea Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Dar es Salaam. (Wa kwanza kushoto) ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (wa kwanza kushoto) akizungumza na Kamishna wa Operesheni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage (wa kwanza kulia) pamoja na maafisa wa Jeshi hilo, mikakati ya kudumisha uhusiano baina ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Benki ya CRDB, wakati wa kikao na Uongozi wa Benki ya CRDB, walipotembelea Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Dar es Salaam.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Peter Mabusi, akifafanua jambo kwa Uongozi wa Benki ya CRDB, wakati wa kikao walipotembelea Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Dar es Salaam. (Wa kwanza kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei na (wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Operesheni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage.
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage (watano kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (mwenyesuti nyeusi), Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waliombatana na Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo na Viongozi Waandamizi wa Benki ya CRDB, jijini Dar es Salaam.
habari na Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...