Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), Dkt. Agnes Kijazi (kulia), akifafanua
jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati Kamati hiyo
ilipokuwa kwenye ziara ya kujifunza namna mamlaka hiyo ivyofanya kazi. Katikati
ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Seleman Kakoso na wa kwanza kulia ni Naibu
Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), Dkt. Agnes Kijazi akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Seleman Kakoso, wakati kamati hiyo ilipotembelea mamlaka hiyo kukagua namna inavyofanya kazi, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi, Aunyisa Meena (kushoto), kuhusu namna walivyojipanga kuimarisha miundombinu ya miradi ya hali ya hewa kwa mwaka mpya wa fedha 2018/2019, wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miudombinu ilipotembelea Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Seleman Kakoso, akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), Dkt. Agnes Kijazi (katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo Dkt. Buruhani Nyenzi (kushoto), wakati kamati hiyo ilipotembelea mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...