*TRA yawataka wafanyabiashara wenye changamoto za kikodi kufika ofisini

NA RACHEL MKUNDAI, DODOMA
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere, amewataka wafanyabiashara wote nchini ambao wanakutana na changamoto za kikodi kuwasiliana na ofisi za TRA zilizo karibu nao ili ziweze kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

Kamishna Kichere ameyasema hayo alipotembelea kiwanda wa DI&PC kinachotengeneza vinywaji kilichopo jijini Dodoma na kuongeza kuwa TRA ipo tayari kusikiliza changamoto zozote za kikodi kutoka kwa wafanyabiashara na itazifanyia kazi kwa kushirikiana na wafanyabiashara hao ili kuhakikisha kuwa serikali inapata mapato na wafanyabiashara wanalipa kodi zao kwa wakati. 

“Wafanyabiashara wale wenye changamoto za kikodi waje, tukae tuongee nao, na tuone namna ya kuzishughulikia na wafanyabiashara walipe kodi kwa wakati, tusonge mbele”, ameongeza Kamishna Mkuu wa TRA”, amesema Kamisha Kichere

Naye mmoja wa wakurugenzi wa kiwanda hicho Katherine Mwimbe, amesema ujio wa Kamishna Mkuu wa TRA katika kiwanda hicho umeleta faraja kwao kwa sababu wamepata fursa ya kuwasilisha kwake moja kwa moja changamoto za kikodi walizokuwa nazo na Kamishna amewahakikishia kuzifanyia kazi haraka.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akiwa katika kikao na uongozi wa Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma, wakati alipofanya ziara yake ya kikazi kiwandani hapo kusikiliza changamoto zinazowakumba Wafanyabiashara.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akizungumza na mmoja wa Wakurugenzi wa Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma, Bibi. Catherine Mwimbe wakati alipofanya ziara yake ya kikazi kiwandani hapo kusikiliza changamoto zinazowakumba Wafanyabiashara.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kushoto) akizungumza na Wakurugenzi wa Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma mara alipokamilisha ziara yake ya kikazi kiwandani hapo kusikiliza changamoto zinazowakumba Wafanyabiashara.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akiwa pamoja na viongozi wengine wa TRA wakitazama shamba la mizabibu ambalo ni mali ya Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi kiwandani hapo kusikiliza changamoto zinazowakumba Wafanyabiashara.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma, Bibi. Catherine Mwimbe wakitazama miundimbinu ya kiwandani hapo wakati wa ziara yake ya kikazi kusikiliza changamoto zinazowakumba Wafanyabiashara.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...