Na Sophia Mtakasimba(TaSUBa)

Kanisa la waadiventista Wasabato Tanzania limeishukuru Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa kutoka nafasi kwa wanamuziki wa kanisa hilo kujifunza Muziki katika taasisi hiyo,kupitia program maalumu ya Kozi fupi ya Muziki ya mwezi mmoja iliyoanza tarehe 1 Julai na kuhitimishwa leo.

Akizungumza katika ufungaji wa program hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa TaSUBa Bagamoyo, Mhazini wa kanisa la wasabato kutoka Jimbo la Kusini mwa Tanzania ,Mchungaji January Athanas Sigome amesema kuwa kanisa linaishukuru Sana TaSUBa kwa kutoa nafasi kwa Waimbaji ,Viongozi na watunzi wa nyimbo kutoka makanisa ya Waadventista wasabato,kujifunza Muziki na anaamini wahitimu wataenda kuwa chachu ya mabadiliko katika makanisa yao.

Aliongeza kuwa kanisa liliamua kushirikiana na TaSUBa kuendesha program hiyo ili kuwafanya watenda kazi wake wajifunze muziki na kuweza kurejesha heshima ya ibada kwa Mungu kama ilivyo katika maandiko matakatifu ,maana katika nyakati za sasa kumekuwepo na mkanganyiko mkubwa juu ya namna bora ya kurejesha ibada ya sifa kwa Mungu.

Aidha Bw.Sigome alisema kuwa kanisa limeichagua taasisi ya sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)kwa kuwa ndio sehemu pekee yenye wakufunzi wenye weledi wa kutosha pamoja na vifaa vya kufundishia vya kutosha.

Nae Leonard Busee ambaye ni mhitimu wa program hiyo amesema kuwa wakiwa TaSUBa wamejifunza mambo mengi ambayo awali walikuwa hawayajui ikiwemo upigaji wa vyombo vya muziki,Falsafa ya muziki ,kusoma muziki pamoja na ufundi wa sauti

Nae mtendaji mkuu wa TaSUBa Dkt.Herbert Makoye amesema kuwa ,kozi hiyo maalumu ni miongoni mwa program mbalimbali ya kimafunzo ambayo TaSUBa inatoa kwa makundi maalumu kulingana na mahitaji yao.Pia kozi za muda mrefu za Stashahada na Astashahada katika fani za mbalimbali zinaendelea kutolewa na sasa milango ipo wazi kwa wanaohitaji kutuma maombi ya kujiunga na chuo.
Mhitimu mwenye umri mdogo kuliko wote , msichana Naomi Yonazi akipotea cheti cha ushiriki wa program maalumu ya muziki.
Mtendaji mkuu wa TaSUBa Dkt.Herbert Makoye (wa pili kushoto), pamoja na Mhazini wa kanisa la waadventista wasabato Jimbo la kusini mwa Tanzania Mchuganji January Atanas Sigome (anayefuata baada ya Dkt.Makoye ), wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa program maalumu ya mafunzo ya muziki .
Wahitimu wa Programu maalumu ya mafunzo ya muziki wakiimba katika hafla ya ufungaji wa mafunzo.
Wakufunzi wa TaSUBa walioendesha program maalumu ya mafunzo ya muziki wakiwa katika picha ya pamoja, kutoka kushoto ni Heri Kaare,Rhoda Mitanda,Peter Zengo,Melkiades Banyanka na John Sagati .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...