Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mara nyingine tena, imeipiga kalenda kesi ya Uhujumu uchumi inayomkabili, Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Habinder Seth na mwenzake James Rugemalira imeahirishwa hadi Julai 19/2018 sababu upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Wakili Serikali Mwandamizi, Mtalemwa Kishenyi  akisaidiana na wakili kutoka Takukuru, Leonard Swai, alidai mahakamani hapo kuwa, kesi hiyo leo imekuja kwa kutajwa na kuiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo kwani upelelezi bado haijakamilika.

Alidai kuwa wapo kati hatua za mwisho kukamilisha upelelezi.

Kufuatia maelezo hayo, wakili wa utetezi, Hajra Mungula akisaidia na Dora Malaba, waliutaka upande wa mashtaka kuhakikisha upelelezi unakamilika kwa wakati, ili kesi iweze kuendelea.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi, anayesikiliza kesi hiyo, ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 19, 2018.

Sethi na Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka  12 ya  uhujumu uchumi  kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kughushi,  kutoa nyaraka za kughushi.

Pia wanadaiwa kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu,  kutakatisha fedha  na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...