Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
Upande wa Mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi, inayowakabili vigogo wanne wa Kampuni ya Six Telecoms Limited na kampuni yenyewe umeileza Mahakama kwamba jalada la kesi dhidi ya washtakiwa hao lipo mikononi kwa (DPP) ambaye atatoa hatma ya kesi hiyo kusikilizwa ama la.
Wakili wa Serikali, Patrick Mwita ameeleza hayo leo, Julai 5, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.
Mwita alidai wakili wa Serikali Jackline Nyantori anayeendesha kesi hiyo, alimpatia taarifa kuwa hadi Jana jalada la kesi lilikuwa bado linapitiwa na DPP.
Kufuatia taarifa hiyo, Hakimu Simba alisema kesi hiyo ni ya muda mrefu na akasisitiza jalada hilo lifanyiwe Mkazi haraka ili liweze kukamilika. Kesi imeahirishwa hadi Julai 20,2018.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mwanasheria na Mhadhiri na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Ringo Tenga, Mhandisi na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Six telecoms, Hafidhi Shamte, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms Limited.
Washtakiwa katika kesi hiyo wanakabiliwa na mashtaka sita ya utakatishaji wa fedha na kuisababishia TCRA hasara USD 3,748,751.22, sawa na Sh 8 bilioni za kitanzania.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...