Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa yupo tayari kuwajibu watu wote ambao wataonekana kubeza ujio wa ndege mpya ya Boeing 787-8 Dreamliner.

Makonda ametoa kauli hiyo leo wakati anatoa utambulisho kwa Rais Dk.John Magufuli kuhusu baadhi ya wageni waliofika kushuhudia tukio la ujio wa ndege hiyo.

Hivyo ametumia nafasi hiyo kutoa ombi kwa Rais Magufuli kutowajibu wote ambao watabeza ujio wa ndege hiyo katika mitandao ya kijamii na kwamba kazi ya kuwajibu ataifanya yeye na kuungwa mkono na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

“Naomba nitoe ombi kwako Rais umekuwa ukitufanyia mambo makubwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.Hata hivyo nikuombe usiwajibu watu ambao watabeza ,kazi hiyo nitaifanya mimi tena kwa kuwafuata huko huko mitandaoni.“Rais ukiwa pale Ikulu endelea tu na mipango yako ya kuwafanyia maendeleo Watanzania wote, hili la kuwajibu wanaobeza mambo makubwa ambayo unayafanya tutafanya sisi,”amesema Makonda.

Amemsifu Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo ambayo Watanzania wanayoana na wale ambao hawataki kuyaona basi watege masikio yao vizuri.“Ndege hii najua leo itakuwa kwangu na baadae itakwenda Mwanza, Arusha na Mbeya.Hata hivyo ndege hii itakwenda zaidi ya Bara la Afrika.

“Yoyote ambaye anapinga kinachofanyika maana yake anapingana na ukweli.Kuna mafanikio makubwa yanaonekana na ambaye haoni basi atege masikio yake vizuri asikie,”amesema Makonda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...