Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAZAZI na Walezi nchini wameshauriwa kutowafungia ndani watoto wenye ulemavu wa aina yoyote ile na badala yake wahakikishe wanaacha watoke nje na kubwa zaidi wapatiwe haki zao za msingi ikiwamo ya elimu.

Amesema watoto wenye ulemavu wakiwezeshwa wanaweza kufanya mambo makubwa yakiwamo ya kutimiza ndoto zao, hivyo kuwafungia ndani ni kuwanyima haki zao za msingi, hivyo jamii yenye tabia hiyo ni vema wakaiacha.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Mke wa Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) wakati akizungumza na walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mchanganyiko Kariakoo jijini Dar es salaam.

Mama Salma alikuwa mgeni rasmi katika tukio la kukabidhi msaada wa vifaa vya kufundisha zikiwamo Laptop maalum kwa wanafunzi wenye ulemavu waliopo shuleni hapo. Msaada huo umetolewa na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasem Al-Najem.Hivyo Mama Salma ametumia nafasi hiyo kuwashauri wazazi na walezi ambao wana watoto wenye ulemavu wa aina yoyote ile kutowafungia ndani.

“Kitendo cha kumfungia mtoto ndani kwasababu ya ulemavu alionao si jambo nzuri na wala halimpendezi Mwenyezi Mungu kwani mtoto hakuomba kuwa alivyo.Pia kumfungia mtoto ndani unamfanya ashindwe kukua kutokana na kukosa miale ya jua na hasa ya nyakati za asubuhi.

“Nitoe rai watoto wenye ulemavu waachwe wawe huru na wapewe haki zao za msingi ikiwamo elimu ambayo ndio msingi wa maendeleo yake ambayo yatamfanya atimize ndoto yake.Tuwaendeleze watoto wenye ulemavu kufikia malengo yao,”amesema Mama Salma.
 Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al- Najem, akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa  mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi  walemavu  shule katika shule ya  Msingi Uhuru Mchanganyiko, vyenye thamani ya shilingi milioni 80.picha na Emmanuel Massaka (Globu ya jamii).
 Balozi wa Kuwait nchini,  Jasem Al- Najem na Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mama Salma Kikwete,wadau mbalimbali wa elimu wakikagua vifaa hivyo walivyo vikabidhi katika shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko vitakavyo wasaidia walemavu katika masomo yao,jana jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akizungumza  katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...